Kampuni
ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imedhamini Mbio za Sita za
Ngorongoro Marathon zenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria
zinazotarajiwa ‘kutimua vumbi’jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu katika
mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Ufunguzi wa mbio hizo utafanywa na
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.
Meneja
Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kuwa, kwa mwaka huu kampuni
hiyo imetoa fedha taslimu, simu za kisasa kabisa za mkonaoni pamoja na
muda wa hewani kwa mshindi wa kwanza wa kundi la wanaume na mshindi wa
kwanza kwa kundi la wanawake.
“Tigo
kwa kuwajali Watanzania, tumeona umuhimu mkubwa sana wa kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambapo dhidi ya malaria ambayo
imekuwa ikipoteza maisha ya watu wengi wa rika mbalimbali kupitia mbio
hizi…” alifafnua Mpinga. Kwa
upande wake Mratibu wa ZARA Charity ambao ndio waandaji wa mbio hizo
Bw, Datus Joseph alifafanua kuwa, pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya
malaria, mbio za Ngorongoro Marathon pia zinasaidia kukuza utalii wa
ndani na nje ya nchi.
“Mbio
hizi ni za Sita tangu kuanzishwa kwake na Tigo wameendeea kutupa
‘support’ na tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa wadhamini wetu…”
alifafanua Joseph. Aliendelea kufafanua kuwa, ZARA Charity inawashukuru wadhamini mbalimbali wa mbio hizo ambazo zimekuwa za mafaniko makubwa.
No comments:
Post a Comment