Ndoa
za baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinadaiwa
kuwaka moto kufuatia kuibuka kwa wimbi la madadapoa raia wa Rwanda
ambao wamekiri kuwapa uroda waheshimiwa hao wanapokuwa mjengoni,
Dodoma,Uchunguzi umebaini kuwa, wake wa waheshimiwa hao walipata
mshtuko mkubwa hivi karibuni kufuatia taarifa ya kukamatwa kwa
machangudoa hao, Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na
Ziada Mukamurera (25) huku wawili kati yao wakikutwa na dawa za
kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARVs).
CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, taarifa za
kukamatwa kwa machangu hao ziliwafanya baadhi ya wake hao wa wabunge
kuwa na mashaka makubwa juu ya maambukizi ya VVU kutokana na ‘wauza
sukari’ kukutwa na dawa hizo.
“Kwa kweli ndoa zao zimetikisika sana,
wake wa wabunge wamepandwa na presha, wamekosa amani, wanahofia na wao
wameambukizwa kwani ni dhahiri machangu hao wamekuwa wakionekana Dodoma
kipindi cha Bunge au Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM),” kilisema chanzo chetu.
MAMA WA MHESHIMIWA
Mmoja
wa wake wa waheshimiwa aliyezungumza na Ijumaa kwa sharti la kutotajwa
gazetini alisema kuwa dawa sasa hivi hakuna kuwaacha waume zao waende
wenyewe mjengoni bali ni kuambatana nao kwani hali si shwari.
Taarifa
zaidi zilidai kuwa, machangu hao waliokuwa wakiishi katika nyumba moja
ya kulala wageni iliyopo maeneo ya Area D, mjini Dodoma, wamekuwa
wakifanya biashara hiyo katika klabu za usiku ambazo waheshimiwa nao
huingia kujirusha.
WABUNGE WANASEMAJE?
Akizungumzia
wimbi hilo la machangu mjengoni, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu
(CCM), alisema yeye haliwezi kumgusa kwa sababu si mtu wa kujirusha.
“Mimi siyo mtu wa viwanja, ningekuwa nakwenda hapo sawa, ningeweza kuwazungumzia. Waulizwe wanaokwenda kujirusha,” alisema.
Naye
Mbunge wa Mbinga, John Komba (CCM) alisema: “Dodoma nina nyumba yangu,
sikaagi hotelini mimi wakati wa bunge. Sasa hao machangu nitakutana
nao wapi? Nikitoka bungeni breki ya kwanza ni nyumbani kwangu. Waulizwe
wabunge wanaoenda kwenye kumbi za starehe.”
TAMKO LA BUNGE
Kuhusiana
na madai hayo ya maambukizi ya VVU kwa waheshimiwa, Mkurugenzi wa
Masuala ya Bunge, John Joel aliliambia Ijumaa kuwa wabunge wote
wanatambua namna ya kujikinga na maradhi hayo na wana kitengo maalum
kinachoshughulikia utoaji wa elimu ya maambukizi ya ugonjwa huo hivyo si
rahisi kuambukizwa.
Source Global Publisher
No comments:
Post a Comment