MSANII
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya aliyetambulika kwa jina moja la
Rocky mkazi wa Kawe, Dar amefariki dunia baada ya kujidunga madawa ya
kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo na kuomba hifadhi ya jina lake, marehemu anayekadiriwa kuwa na umri wa
Ray C
miaka
23-27, alipatwa na mauti Machi 27, mwaka huu baada kunywa vidonge kumi
vya dawa za kulevya aina ya Valium kisha kujidunga sindano tatu za
Cocaine.
Langa
Chanzo
hicho kilidai, marehemu alikuwa akionywa mara kwa mara na ndugu zake
lakini alikuwa akikaidi hali ambayo ilisababisha akamatwe na kuswekwa
jela kwa miezi kadhaa kabla ya kuachiwa.
“Marehemu alitoka Segerea juzi Jumatatu (Machi 25) na Jumanne akaanza kutumia tena dawa za kulevya kama kawaida, akajidunga vidonge kumi kwa mpigo.
“Marehemu alitoka Segerea juzi Jumatatu (Machi 25) na Jumanne akaanza kutumia tena dawa za kulevya kama kawaida, akajidunga vidonge kumi kwa mpigo.
Aisha Madinda
“Akaweka
kete tatu kwenye bomba la sindano tayari kwa kujidunga ndipo
alipozidiwa na kupatwa na umauti akiwa bado hajakamilisha zoezi hilo,’’
kilidai chanzo hicho.
Kabla ya marehemu hajazikwa katika makaburi ya Kawe, askari walifika katika eneo hilo ambapo walibainisha kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutumia madawa ya kulevya katika eneo hilo.
Kabla ya marehemu hajazikwa katika makaburi ya Kawe, askari walifika katika eneo hilo ambapo walibainisha kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutumia madawa ya kulevya katika eneo hilo.
“Vijana
wengi hapa Kawe wamejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Tunawashauri hasa hawa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao
walitangaza kuacha basi waache kweli maana wakirudia basi kifo
kinawaita.
Msafiri Diof
“Historia
inaonesha kuna wimbi kubwa la wasanii ambao wamekuwa wakitumia madawa
ya kulevya kwa siri kubwa,” alisema afisa mmoja wa polisi aliyeomba
hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji.
No comments:
Post a Comment