Amani
usiamini! Bibi kizee Veronica Amos Kayombo (76), mwenyeji wa Ludewa,
Njombe anayeishi Buza, Dar, amedai kuisikia sauti ya Mungu ikimuagiza
akaonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete ampe ujumbe muhimu, shuka nayo.
MAHOJIANO MAALUM
Akizungumza
katika mahojiano maalum mwanzoni mwa wiki hii akiwa
nyumbani kwake Buza, Bibi Veronica alisema amekuwa akitokewa na Mungu
mara kwa mara na kumpa maelekezo mengi ambayo anatakiwa kuyatoa pale
atakapofika kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.
ATOKEWA NA TASWIRA YA MUNGU
“Nimekuwa nikitokewa na taswira na sauti ya Mungu, kwa idadi inaweza kufika mara saba na kuambiwa
kuwa
nisiondoke Dar, bila kuonana na Kikwete ili nimpe zawadi zake ambazo
nimezitunza kwa muda mrefu na siri iliyoko moyoni ambayo nimepewa na
Mungu,” alisema bibi kizee huyo.
KWA NINI JK?
Aliendelea
kusimulia kwa masikitiko kuwa zawadi atazompatia JK ni kwa ajili ya
kumpongeza kwa kuweza kuwasaidia albino, watu wasiojiweza, wazee na
kutuliza vita nchini Kenya na Uganda ambazo zilikuwa zimejifichwa kwani
nchi nyingine kama Rwanda na Burundi zilikuwa wazi.
ANATOKEA NJOMBE
ATUMIA MKWANJA MREFU
Baada
ya hapo amekuwa akifanya jitihada za aina mbalimbali kwa ajili ya
kuonana na rais lakini hadi sasa hajafanikiwa kwani ameshapoteza fedha
nyingi kwa kuwahonga watu ili wamfikishe Ikulu pale Magogoni, Dar na
kutoa kopi za barua kwa ajili ya kuomba maombi ya kukutana naye.
“Nimepoteza
fedha nyingi sana kila ninayekutana naye ananiambia atanipeleka lakini
nimpatie fedha, natoa mpaka sasa nimeishiwa, nimeshaenda mpaka ofisi
zote zinazohusika na kuwakutanisha watu na rais lakini sikufanikiwa,
watu wamekuwa wakiniona chizi lakini nina akili zangu timamu na maono
haya ni ya Mungu kwani mbali na kuambiwa pia la kufanya nikifika huko
lipo kwenye kitabu hiki (anaonesha Biblia).
Bibi
kizee huyo alipoona ameshahangaika huku akizuia kila mara kuingia
Ikulu, aliamua kuita vyombo mbalimbali vya habari na kufikisha ujumbe
wake ambapo mbali na hapa gazetini pia radio zitarusha matangazo yake
moja kwa moja yatamfikia Rais Kikwete.
AMPA ZAWADI LOWASSA, MKAPA
Kwa
mujibu wa bibi Vero, aliwahi kukutana na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward
Lowassa ambaye alimpatia gunia la mahindi na zawadi za Rais wa Awamu ya
Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Ana Mkapa alipokuwa kwao Njombe.
Kumbukumbu
zinaonesha kuwa mama huyo wakati anatoa zawadi hizo alioneshwa kwenye
vyombo vya habari ambapo alitoa kitenge cha mama, gunia la mahindi na
zawadi ya rais huyo mstaafu.
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment