Wednesday, April 03, 2013

PINDA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU

 

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha  kutokana na  kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha. 

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za uchimbaji katika eneo hilo.

Hatua hiyo ya Pinda imetokana na ajali ya watu 14 waliopoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi juzi, wakati wengine wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazonyesha jijini Arusha.
Pinda alitoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo pamoja na kuwajulia hali majeruhi wawili waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mt Meru
CHANZO:MWANANHI.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...