Rais mteule wa
Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa
kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo
kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.
Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.
Lakini
katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza
kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili
mchana. Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.
Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua
kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa
habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda
uchaguzi .
Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na
CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali
madai hayo akisema ni ya ''ujinga''. Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi. Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment