Wednesday, May 14, 2014

WACHIMBA MADINI 200 WAFARIKI UTURUKI

157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 200 na kujeruhi wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Waziri wa kawi, Taner Yildiz, amesema kuwa zaidi ya wafanyikazi 780 walikuwa katika mgodi huo pale kuliposikika mlipuko katika kitengo cha kusambazia umeme.
Waokoaji wanajaribu kila mbinu kuwafikia mamia ya wachimba migodi.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 780 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao .
Bado idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika.
Mgodi huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Jamaa za wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na kububujikwa na machozi.
Waziri wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.
Amesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.
Baadhi yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...