MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Juma
Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amegongwa na gari wakati akifanya mazoezi ya
kutembea kufuatia ugonjwa wake wa kiharusi.
Tukio hilo
lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Kariakoo, Dar ambapo gari hilo
aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga kidogo na kumsababishia
michubuko kwenye miguuni na kichwani.
Dereva wa gari hilo alifanya
uungwana kwa kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu
zake walitaarifiwa na kwenda kumchukua.
“Mzee Kankaa alitoka nyumbani na
kutuaga kuwa anakwenda kufanya matembezi. Tulijua ni karibu, lakini
baadaye tukasikia taarifa kuwa amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi
Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto wa Kankaa.
chanzo : GPL
No comments:
Post a Comment