Monday, December 30, 2013

MAALIM SEIF: "WAZANZIBAR WANATAKA MAMLAKA KAMILI"

maalim1 1e311
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Wazanzibar wanaisubiri kwa hamu Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona kama imezingatia masilahi na matakwa yao katika kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.
Msimamo huo ameutoa kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, Mkoa wa Kalazini Unguja na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Aidha, katika mkutano huo, kwa mara ya kwanza Waziri wa zamani wa SMZ na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Mansoor Yussuf Himid alihutubia tangu avuliwe uanachama wa CCM kutokana na madai ya kwenda kinyume na sera, maadili na nidhamu ya chama hicho.
Katika maelezo yake, Maalim Seif alisema wanachodai Wazanzibar
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
Alisema Zanzibar ilikuwa taifa huru lililoungana na Tanganyika kwa ridhaa na siyo mateka wa Tanganyika, hivyo wanayo sababu ya kujitegemea.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz
"Madai yetu yako wazi, hayana kificho na siyo mageni, tunaisubiri kwa hamu rasimu ya Jaji Warioba, kama ni supu isiyolika, hatutaila tutamrudishia mwenyewe na kuendeleza madai yetu," alisema Maalim Seif.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, alisema Zanzibar itasimama wenyewe na kujiendeleza kwa kufuata misingi iliyowekwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.
"Madai yetu ni kama meli iliyobeba watu wengi, ikizama tunazama wote, lengo letu ni kufika salama katika bandari ya matumaini na kila mmoja aweze kunufaika na matunda ya nchi yake," alisema Maalim Seif.
Alisema ikiwa Wazanzibari watapata Serikali, anaamini mengine yatakuja yenyewe na kuinufaisha Zanzibar kiuchumi na kusisitiza kuwa muundo wa Serikali mbili umepitwa na wakati. 
Chanzo: mwananchi
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...