Sunday, December 22, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MWENYEKITI WA YANGA YUSUPH MANJI BAADA YA KUFUNGWA NA SIMBA JANA


Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea. https://www.facebook.com/jambotz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...