Sunday, December 22, 2013

MWIGULU NCHEMBA AMWONYA SPIKA WA BUNGE


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.
Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumu.
Mkuya katika maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu kwa mtu mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17.
Katika mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.
"Naomba tukubaliane katika kubana matumizi, na hivyo ninakuomba Mheshimiwa Spika tuanze na ofisi yako achana na kutoa fedha kwa kuwapa wabunge kwa ajili ya kwenda Dubai kwa burudani,"alisema Nchemba.
Alisema umefika wakati ambao Serikali inatakiwa kufanya uamuzi wa kutumia fedha katika mambo muhimu ambayo yanaigusa jamii kuliko mambo ambayo hayana maana. Kwa upande mwingine aliwalaumu watendaji kuwa wameiangusha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kutoa ushauri na usimamizi mzuri katika makusanyo ya kodi.
Kwa upande wake Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliinyooshea vidole Serikali kuwa ndiyo iliyovuruga mchakato mzima wa makusanyo ya kodi ambayo muswada wake ulishapitishwa.
Mbatia alitoa sababu kuwa ndani ya Serikali wamekuwa wakiamua mambo lakini kwenye utekelezaji wake wanagawanyika.
Chanzo:Mwananchi

Kuwa wa kwanza kupata habari kwa ku-Like page Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...