Tuesday, December 24, 2013

WANAMUZIKI WA KUNDI LA PUSSY RIOT WAACHIWA HURU

Wanamuziki wote wa kundi la muziki wa Punk la Pussy Riot la nchini Russia wameachiliwa huru kutoka gerezani chini ya sheria ya msamaha.
Nadezhda Tolokonnikova aliachiwa huru kutoka hospitali moja ya gereza lililopo Siberia, wakati mwenzake Maria Alyokhina aliachiliwa huru Jumatatu huko Nizhny Novgorod.
Wote wameuita msamaha huo kuwa ni sawa na sarakasi za serikali za kujisafisha kabla ya kufanyika kwa michezo ya olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika Russia Februari mwakani.
Wanawake hao wanamuziki walifungwa Agosti 2012 baada ya kuimba nyimbo inayokejeli katika kanisa kuu jijini Moscow.
Kitendo chao kilitafsiriwa kama kumkufuru mungu na wananchi wengi wa Russia lakini kutiwa kwao hatiani kwa kosa la utukutu ukichochewa na chuki dhidi ya dini ulishutumiwa na vikundi vya kutetea haki za binadamu, wanaharakati wanaompinga Rais Vladmir Putin na mataifa ya nje.
Watu wengi wanaotumikia vifungo wanauona msamaha huo kama jaribio la Rais Putin la kusafisha taswira yake katika nchi za magharibi na kuiboresha rekodi yake ya haki za binadamu kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki huko Sochi Februari 2014.
Siku mbili baada ya sheria hiyo ya msamaha kuanza kutumika, Rais Putin alimsamehe Mikhail Khodorkovsky, ambaye siku za nyuma alikuwa ni mtu anayeongoza kwa utajiri nchini Russia na mkosoaji binafsi wa sera za serikali, hatua ambayo pia ilitafsiriwa kama kuyaridhisha mataifa ya magharibi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...