Wanasiasa
wawili wa bunge la Kongres la Chama cha Republican nchini Marekani
wamehoji iwapo ziara ya wanamuziki maarufu wa nchi hiyo mume na mke Jay Z
na Beyonce nchini Cuba ilikuwa na kibali cha serikali.
Mastaa
hao wamepigwa picha kadhaa wakiwa mjini Havana wakisalimiana na
mashabiki wao, wakitoka kupata msosi na kutembelea sehemu kadhaa za mji
huo wakati wakisherehekea miaka mitano ya ndoa yao.
Hata
hivyo vikwazo vya kibiashara vya Marekani vinazuia wamerekani
kuitembelea Cuba kwa sababu za kiutalii pekee na anayetaka kusafiri
lazima aombe kibali maalum.
Wanasiasa
hao Ileana Ros-Lehtinen na Mario Diaz-Balart wametuma barua kwa Idara
ya hazina ya Marekani wakiulizia ni aina gani ya kibali walichopewa
wanamuziki hao kuitembelea nchi hiyo.
Wamesema
vikwazo vya kuitembelea nchi hiyo viliwekwa kwa sababu marekani
iliiorodhesha serikali ya Cuba kama taifa linalounga mkono ugaidi na
kudai kuwa nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye rekodi mbaya ya
ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa
kawaida sababu za muhimu zinazoweza kumruhusi raia wa Marekani kwenda
Cuba ni pamoja na matibabu, kusoma, sababu za kidini, huduma za kijamii
na sababi nyingine za kibinadamu.
No comments:
Post a Comment