Thursday, June 20, 2013

MSIKILIZE MBUNGE ALLY KEISSY WA NKASI ANAYEWAVUNJA MBAVU WABUNGE

Stori ya kwanza ni ya Mbunge wa Nkasi Ally Keissy June 18 2013 bwana alivunja rekodi ya kuwa mbunge aliechekesha watu wengi wakiwemo wabunge bungeni, sio tu kwa sababu ya kutoa vichekesho lakini pia ni kwa namna alivyokua akieleza mambo pamoja na kuikosoa Serikali.
.
Mbunge wa Nkasi Ally Mohamed Keissy.


Anakwambia ‘Twende Kigoma, Mwanza, Tabora, Mpanda, Shinyanga tuwaulize watu mnataka reli au viwanja vya ndege… mtashangaa wenyewe, vipaumbele gani mnapeleka viwanja vya ndege? mtu gani wa Tabora anapanda ndege kama sio Mbunge, DC na Mkuu wa mkoa… ? ni Treni…… hawataki viwanja vya ndege, viwanja vya ndege baadae…. 

kwanza ndege zenyewe zikwapi? mna ndege nyie???? mabilioni ya hela mnajenga viwanja vya ndege… ndege hatuna, wapanda ndege ni nyie wenyewe Wabunge na Mawaziri… jamani tutulie tuweke vipaumbele ambavyo vinaweza kusaidia Wananchi na uchumi wa nchi,  mtapakia mizigo, madebe mawese kwenye ndege? migebuka kwenye ndege? acheni mambo ya kurukiakurukia ndege zenyewe hamna”

“Mmefilisi shirika la ndege tunawaambia tuwakamate wale waliofilisi tuwafunge pingu zao, sasa sheria mpya kama wamekufa tuwafufue tuwasage mifupa yao… mi nashangaa baadhi ya Wabunge hapa wanakuja tuondoe hela hii tuondoe hela hii… utapata wapi hela ya kuiendeleza nchi yako? leo Uingereza kodi ya TV unalipia, ukiwa nazo tatu utalipia kila moja… wewe una TV mpaka 10 mpaka chooni, umekaa hulipii chochote… nani akudai? ” – Keissy

“Mafisadi wanajulikana, hata mzee Sitta nimemsikia siku moja akisema hawa dawa yao kuwanyonga….. mimi Mbunge hapa, baada ya mwaka nina gorofa 10 nimepata wapi hela? sijakwenda benki sijakwenda popote, hapohapo ndio pa kunibana… na hizi pesa zinazochangiwa kwenye maharusi mabilioni ya hela, michango ya kanisa na Misikiti zikatwe kodi 30% palepale… wauza dawa za kulevya kama hawajakamatwa lakini wana majumba, wakatwe kodi.. shida yetu kodi sisi hatujui dawa zako umepeleka wapi huko tumeshindwa kukukamata lakini tulipe kodi” – Mbunge Keissy

“Tukipata maafa kidogo… kelele misaada, tukisema kodi mnapiga kelele nyie Wabunge… Ebooooo? itakuaje? nani ameoa Mwanamke nyumbani kwake anakwenda kuomba msaada kwa jirani? watakuchukulia mke wako… JITEGEMEE!!!!!”
Watu mbavu hawana…… unaweza kumsikiliza mwenyewe hapa chini upate uhondo wote.
Sauti yake ipo hapa soundcloud.com

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...