Thursday, June 20, 2013

MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN AFARIKI DUNIA




Na Steven Kanyeph.
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha chanel Ten CHARLES HILILA amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospital ya Mkoa wa Shinyanga.

Marehemu Charles Hilila alilazwa katika hospital ya mkoa tarehe kumi mwezi june mwaka huu akisumbuliwa na maradhi ya TB ya mifupa ambapo tarehe kumi na sita mwezi huu alihamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi mpaka mauti yalipomchukua .


Kwa mujibu wa mke wa marehemu amesema kuwa mazishi yatafanyika katika kijiji cha Jomu Tinde mahali alipozaliwa marehemu yakitanguliwa na misa takatifu ya mazishi itakayofanyika katika kanisa kuu la mama mwenye huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.

Marehemu Hilila ameacha mjane mmoja na watoto watatu, wakike mmoja na wakiume wawili.

Marehemu Hilila enzi za uhai wake alifanya kazi katika kituo cha televisheni cha chanel Ten lakini aliwahi kufanya kazi katika kituo cha matangazo cha radio Faraja. Mungu alaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...