Sunday, October 12, 2014

POSHO ZA BUNGE ZAIBUA MAPYA


Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta. PICHA|MAKTABA

Siku chache baada ya Bunge la Maalumu la Katiba kumaliza muda wake, matumizi ya fedha zilizobaki kwenye Bunge hilo yameibua mvutano baada ya kuwapo taarifa kuwa fedha hizo ziliisha, huku Wizara ya Fedha ikieleza kuwa bado zipo.
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Sitta alipotafutwa kutoa ufafanuzi wake simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokewa kwa muda mrefu.
Alipoulizwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye anakaimu uwaziri wa fedha kuhusu maombi ya nyongeza ya fedha, alisema hajapokea maombi ya nyongeza kutoka katika Bunge hilo na kwamba hawajapata mchanganuo wa fedha walizopewa awali.
“Hatujapata mchanganuo wa fedha zilivyotumika. Utakumbuka kuna wabunge ambao hawakuingia. Kwa hiyo tunaamini kutakuwepo na chenji, kwa sababu haiwezekani kukawa na wajumbe zaidi ya 100 hawakuingia halafu bado fedha ikatumika vilevile,” alisema.
Wabunge wa Bunge hilo walikuwa wakilipwa kwa siku posho ya Sh300,000, kati ya hizo Sh70,000 zilikuwa ni posho za vikao, Sh 230,00 zilikuwa ni fedha za kujikimu.
Mwigulu alisema kuwa Bunge hilo lilipewa bajeti ya Sh32 bilioni na kama Rais Jakaya Kikwete angekubali kuongeza siku 24 zingetumika Sh10 bilioni.
Alisema: “Mimi kwa maoni yangu fedha zote ambazo zitabaki iwe kwenye kura ya maoni ama ingeenda kuwasaidia watoto wa maskini waliokosa mikopo ya elimu ya juu,”alisema.
Alisema katika kipindi cha mwaka jana wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na vyuo vikuu wapatao 12,000 walikosa mikopo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Chukua taswira ya wale watoto wamesomeshwa na bibi zao na wajane kwa vipesa vya kuokoteza halafu ikafika wakati wa kujiunga na chuo kikuu akakosa fedha ya mkopo tena sio bure bali ni mkopo,” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo naamini fedha yote tunayoipata ina umuhimu wa kuielekeza kule na wenzangu wizarani bado tunaendelea kubana matumizi ili kila kijana anayefaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu basi awe na uwezo wa kukopa.”
Alisema hali hiyo anaitambua tangu angali mbunge tu Iramba Magharibi na kwamba yeye asingepata mkopo asingeweza kusoma.
“Mimi nisingepata mkopo, ndoto yangu ndiyo ingekuwa ni mwisho wake naamini kwamba leo hii nisingekuwa hapa. Sasa familia za namna hiyo bado zipo,” alisema.
Kwa mujibu wa Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, jumla ya wanafunzi 12,000 ambao walikosa mikopo ya elimu ya juu mwaka jana na mwaka huu mahitaji ni kwa wanafunzi 28,000.
“Kwa hiyo utaona fedha yoyote inayopatikana si ya kufanyiwa luxury (si ya anasa), inatakiwa tuwaangalie kwa jicho la huruma watu hao,” alisema.
Alisema Bunge hilo lilikuwa linajiongezea siku 24 ambazo hazipo katika bajeti.
“Siku 24 zingehitaji zaidi ya Sh10 bilioni. Niliwatahadharisha kwa kuongeza siku 24, kwa kuondoa siku za mapumziko ingefanya Bunge liende hadi tarehe 28,” alisema Mwigulu.
Alisema kwanza ilikuwa ni kinyume cha sheria kwa sababu waraka wa serikali (GN) unasema Bunge liishie Oktoba 4, mwaka huu.
“Lakini pili tunaongeza bilioni 10 kwa wajumbe kupumzika tu. Kwa hiyo angalizo langu ni kuwa mnapoamua siku hizo ziwe za mapumziko mnaongeza siku 24 haziko katika bajeti,” alisema na kuongeza:
“Walikataa lakini namshukuru Mheshimiwa Rais alisema baadaye kuwa Bunge litaishia Oktoba 4. Wakati mwingine ukiwa mdogo wa umri na mwili watu wanaweza kupuuza mawazo yako hata yakiwa mazito. Walipuuza kwamba haina shida wajumbe wanatakiwa wasome,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

 Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...