Sunday, October 12, 2014

MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI ‘ YACHAPWA’ KWA MARA YA KWANZA NA POLAND

Poland imeifunga UJerumani kwa mara ya kwanza na kukwea juu ya kilele katika kundi la Nne kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016 nchini Ufaransa. Mabingwa wa dunia , Ujerumani ilikuwa na rekodi ya kucheza mara 18 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya majirani zao, Poland ambao walipata mabao yote mawili katika kipindi cha pili.
Mshambulizi kinda wa klabu ya Ajax Amsterdam, Arkadiusz Milik, 20 alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 51, na dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Sebastian Mila aliwahakikishia wenyeji ushindi baada ya kufunga bao la pili katika mchezo huo uliopigwa jijini, Warsaw.
Mabingwa hao wa sasa wa dunia, walifungwa mara ya mwisho na Jamhuri ya Czech, Oktoba, 2007 katika michezo ya kufuzu. Ujerumani ilicheza michezo 33 ya kufuzu pasipo kupoteza. Kipa wa Ujerumani, Manuer Neur aliokoa mabao manne ya wazi katika mchezo ambao walishambuliwa sana. Poland iliyokuwa na mshambulizi wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ilipiga jumla ya mashuti 19, huku mashuti 12 yakilenga bao.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alikwenda Poland huku baaddi ya wachezaji wake muhimu wakikosekana. Ujerumani ilibanwa hasa na walimudu kufanya mashambulizi machache . Walipiga mashuti saba tu ambayo yote yalilenga lango lakini nyota wa mchezo huo, golikipa, Wojciech Szczesny alikuwa imara, kipa huyo wa klabu ya Arsenal aliokoa mara 14. Tomas Mueller, Andre Schurrle na Mario Gotze walishindwa kufunga kwa muda wote waliokuwa uwanjani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...