Tuesday, August 11, 2015

DK. BILALI APUUZA UVUMI WA KUIHAMA CCM

MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amekanusha taarifa za uzushi ziliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jana, Katibu wa Makamu wa Rais, Zahor Mohammed Haji kwa niaba ya Dk Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina yake. Zahoro alisema, Dk Bilal yupo nchini Uingereza katika shughuli za ujenzi wa taifa na kwamba hana mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza uzushi huo wana lao jambo.

Katibu huyo amemnukuu Dk Bilal akisema; “Ndugu zangu wa CCM, na Watanzania kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwa taarifu kwamba kuna taarifa inayoenezwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo facebook na whatsApp kuwa nitaitisha mkutano na vyombo vya habari ili kujitoa CCM.
“Taarifa hizo ni uzushi na mzipuuze kwani sina mpango na sifikirii kufanya hivyo kwa sababu sina sababu ya kunifanya niondoke CCM.” 

Aidha, Dk Bilal alisema yupo imara na mwenye siha njema na kuwa hivi sasa anajiandaa kushiriki kikamilifu kuzunguka majimbo yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kumnadi mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli kwa azma ya kumsaidia Rais Jakaya Kikwete aendelee kufanya kazi za kitaifa ili kukipatia CCM ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu ili chama hicho kikongwe kliendelee kukamata dola.

Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii ilikuwa ikisambazwa taarifa ya uzushi. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...