Thursday, June 26, 2014

UBABE BUNGENI, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NUSURA AMPIGE KAFULILA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto) akizuliwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutomfuata Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila baada ya kupandwa na hasira kufuatia mbunge huyo kumtuhumu kwa kumuita mwizi kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Kwa ufupi
“Profesa Muhongo aliliambia Bunge kuwa Serikali ililipa fedha hizo ili kuondokana na kesi hiyo lakini ninazo nyaraka za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuteua kampuni mbili za uwakili kwenda kuiwakilisha katika kesi nchini Uingereza,” alisema Kafulila.


Kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema jana angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. 

Sakata hilo lilitokea jana asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni. Jaji Werema alichukia baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili na mwanasheria huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Waliomzuia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdulla Juma Saadallah.  

Mawaziri hao walimsindikiza Werema hadi nje ya Ukumbi wa Bunge na kutoweka.
Ilivyokuwa Hali ilianza kuchafuka wakati Jaji Werema alipokuwa akijibu mwongozo uliombwa na Kafulila kuhusu fedha za akaunti ya Escrow.  

Katika mwongozo huo, Kafulila alisema Wizara ya Nishati na Madini kupitia Waziri wake, Profesa Sospeter Muhongo alizungumza uongo mara mbili bungeni kuhusiana na fedha za akaunti ya Escrow. “Alisema uongo mbele ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika maeneo mawili, kwamba uamuzi wa kutoa fedha za Escrow kwa IPTL ulikuwa wa Mahakama na Serikali isingeweza kwenda kinyume...” alisema. 

Alisema katika hukumu hiyo ya Septemba mwaka jana, hakuna mstari hata mmoja unaosema kuwa fedha za Escrow wapewe Kampuni ya IPTL. “Profesa Muhongo aliliambia Bunge kuwa Serikali ililipa fedha hizo ili kuondokana na kesi hiyo lakini ninazo nyaraka za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuteua kampuni mbili za uwakili kwenda kuiwakilisha katika kesi nchini Uingereza,” alisema Kafulila.  

Alisema kwamba aliomba mwongozo sababu huo umekuwa mwendelezo wa kuzungumza uongo bungeni... “Naibu Waziri (Nishati na Madini - Stephen Masele), alizungumza uongo bungeni tukaambiwa kuwa wamekutana katika sherehe za kuzaliwa yakaisha, haiwezekani, Bunge ni sehemu ya kuisimamia Serikali. “Haiwezekani Bunge ling’olewe meno liwe ni chombo ambacho mtu anaweza kuzungumza uongo bila kuchukuliwa hatua kwenye jambo hili ambalo linaligharimu taifa mabilioni ya fedha.”  

Baada ya madai hayo, Jaji Werema alisimama na kusema: “Bunge hili liliamua mambo mawili, kwanza kulikuwa suala la rushwa na CAG apewe kazi ya kuchunguza na kutoa taarifa bungeni. La pili kuna watu walitoa vipeperushi humu bungeni, miongoni mwao ni huyu anayetoa maneno machafu (Kafulila),” alisema Werema na kumfanya John Mnyika (Mbunge wa Ubungo-Chadema), kuomba mwongozo uliokataliwa na Mwenyekiti Zungu. 

Hata hivyo, Mnyika na Kafulila waliendelea kuomba mwongozo, lakini Zungu aliwataka wamsikilize Jaji Werema kwa sababu naye alimsikiliza Kafulila. Werema aliendelea: “Suala la Escrow ni suala linalotokana na wanahisa wawili ambao ni IPTL na Mechmar… Pesa ya Serikali haikai kwenye Escrow.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Hata hivyo, alikatishwa na kelele za Mnyika ambaye alitaka mwenyekiti kumpa nafasi ya kutoa taarifa. “Sasa kama unataka kuleta mambo ya nje ndani ya Bunge ningojee pale nje,” Jaji Werema alisema wakati wabunge hao walipokuwa waking’ang’ania kutoa taarifa.  

Alisema ugomvi huo ulitokana na wanahisa wawili hao kila mmoja akitaka IPTL ifilisiwe ili waachane. Alisema Serikali iliingia katika mgogoro huo kwa sababu ya mikataba ya udhamini na kwamba wakati wanagombana iliamua kufungua akaunti ya Escrow.  

Hata hivyo, kuliibuka maneno tena kutoka upande wa Kafulila na Jaji Werema alitaka kusikilizwa hata kama yeye ni mtuhumiwa katika suala hilo. “… Wanyankole wanasema tumbili hawezi kuamua masuala ya misituni… sikiliza tumbili, sikiliza ‘please’ (tafadhali),” alisema Werema. Sentensi hiyo iliamsha kelele kutoka upinzani na Kafulila alisikika akimwita Werema mwizi. Hata hivyo, Zungu alizuia vurumai hizo kwa kumtaka Jaji Werema kukaa na kisha kuwataka wabunge hao wawili kupeleka ushahidi wao Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru).  

Mara tu baada ya Zungu kuahirisha Bunge, Jaji Werema alisimama na kumfuata Kafulila lakini kabla hajamfikia, mawaziri hao walimzuia na kumsindikiza hadi nje. Baadaye, Kafulila na Mnyika waliitisha mkutano na waandishi wakitaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda afute uongo huo bungeni ndani ya siku mbili na akishindwa, watakusanya sahihi za wabunge kumuondoa katika nafasi hiyo. Alipohojiwa kama ni vyema kwa Wassira alisema walimsihi Werema kuachana na Kafulila na kuendelea na shughuli zake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...