Tukio hilo
lilitokea mwanzoni mwa wiki ambapo imeelezwa kuwa Nkamia mbali na kutaka
kumpiga mbunge huyo, pia alimtolea matusi mazito ya nguoni (gazeti hili
haliwezi kuandika).
Kwa mara ya
kwanza mbunge huyo aliingia katika kashfa baada ya kutoa kauli bungeni
kuwa hazungumzi na mbwa, bali anazungumza na mwenye mbwa kabla ya
kuingia katika mzozo na wahariri na baraza la habari aliposema kuwa
Jukwaa la Wahariri na Baraza la Habari ni NGOs za kutafuta fedha.
Uchunguzi wa
Mwananchi ambao umethibitishwa na Nkamia mwenyewe umebaini kuwa chanzo
cha tukio hilo ni kutokana na kuzomewa kwa Nkamia katika kampeni za
uchaguzi mdogo Kata ya Dalai Wilaya ya Chemba.
Kwa mujibu wa
wabunge mashuhuda ambao waliliona tukio hilo, ilielezwa kuwa Nkamia,
ambaye pia ni mwandishi wa habari, alianza kumshushia matusi Moza wakiwa
ndani ya Bunge hadi walipotoka nje alimfuata na kutaka kumpiga.
"Kweli pale
jamaa yetu, alitia aibu, hata hivyo kusema kuwa alikuwa amelewa siyo
kweli maana mimi namfahamu Nkamia vizuri ila ilikuwa ni hasira tu,"
alisema mmoja wa wabunge walioamua ugomvi huo.
Akizungumzia
tukio hilo Moza, alisema kuwa wakati akitoka nje ya ukumbi, alipita
karibu na kiti anachokaa Nkamia na ghafla akaitwa, lakini akashangazwa
na kitendo cha kuanza kurushiwa matusi.
"Kweli Nkamia
na mimi tunatoka wilaya moja, lakini siku ile nilishangaa alinitukana
matusi ya nguoni kabisa ......... (anayataja), lakini mimi kule sikusema
kitu hadi nilipotoka nje alinifuata na mimi hasira ilinishika nikaanza
kumjibu akatupa vitabu ili aje anipige wabunge wenzake wakamkamata,"
alisema Moza.
Alisema kuwa
chanzo cha matusi hayo ilikuwa ni tuhuma kwamba Nkamia alimtuhumu Moza
kuwa aliandaa vijana katika Kata ya Dalai wakati wa kampeni za uchaguzi
wa udiwani ili wamtukane.
"Hata hivyo,
waliomwambia hivyo kwamba niliandaa vijana au nilimtukana walimdanganya
kwani mimi wakati huo nilikuwa bungeni, lakini yeye ndiye
aliyeniporomoshea matusi katika kampeni hizo na ushahidi wa sauti
ninao," alisisitiza Moza.
Kwa upande
wake Nkamia, ambaye kabla ya kuwa mbunge alikuwa mtumishi wa Serikali
katika Shirika la Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) alikiri
kutokea kwa tukio hilo, lakini alikanusha kuingia bungeni akiwa amelewa
kama ilivyoaminika na watu.
Nkamia alitoa
sababu za ugomvi huo kuwa ni kutokana na taarifa kuwa Moza aliandaa
kikosi cha vijana wahuni kulishambulia gari la Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pamoja na kuwazomea viongozi wake akiwemo yeye.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment