Saturday, June 22, 2013

HATIMAE NDUGU YETU MPENDWA CHARLES HILILA AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO



 

 NYUMBA YA MILELE ALIMOLALA MWANDISHI WA HABARI KITUO CHA MATANGAZO CHA CHANELL TEN

Habari Na Steven Kanyeph
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa chaneli ten Charles hilila umezikwa leo katika makaburi ya nyumbani kwao katika kijiji cha Dumida kata ya Tinde mkoani Shinyanga nakuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji akiwemo mkuu wa mkoa wa shinyanga na viongozi wengine wa kiserikali , vyama vya siasa pamoja na viongozi wa kidini.

Mazishi hayo yametanguliwa na ibada ya misa takatifu iliofanyika katika kanisa la mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyangsa na baade kufuatiwa na ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwao na kuongozwa na padre Emmanueli Makolo akisaidiana na padri Josephati Mahalu kabla ya maziko.
katika mahubiri padre Mahalu amewaasa wanajamii kudumisha upendo na kuwakumbusha kuwa kifo kipo mahali popote hivyo wanajamii wanapaswa kumrudia Mungu na kutenda matendo mazuri yenye kuleta amani na yanayompendeza Mungu.


Hali kadhalika mkuu wa mkoa wa Shinyanga Alli Nassoro Lufunga ametoa salamu za rambirambi kutoka katika serikali ya mkoa na kuwaomba wanahabari kudumisha upendo zaidi hasa katika umojawao kwani utawasaidia kufanya kazi kwa weledi na kuleta tija zaidi kwa wanajamii.
Marehemu Charles hilila amefariki juni 19 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa TB ya mifupa uliokuwa unamsumbua .
Aidha marehemu ameacha mjane na watoto watatu ,
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema mbinguni amina

*********************************************************************************


 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...