Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema) Joshua Nassari akiwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), jana, baada ya kuhamishwa kutoka Arusha kwa ajili ya kupata matibabu zaidi baada ya kuumizwa kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni mkoani Arusha.Picha na Silvan Kiwale.
DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.
MBUNGE wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake.
Aidha
amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa
watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna
kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana
na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali.
Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa
na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa
waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe
Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka
jana.
Nassari
aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla
ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard
wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye uchaguzi
wa udiwani wa Kata ya Makuyuni-Monduli.
“Kipigo
nilichopata Lowassa anahusika ananichukia, anataka urais lakini hawezi
kuupata kwa kuuumiza watu kama hivi, alifikiri kwamba nitakufa
sitakufa hadi kwa mapenzi ya Mungu,” alisema.
Alisema
kuna jambo ambalo wananchi wanapaswa kulifikiria ni jinsi ambavyo
kumekuwa na matukio ya kutekwa na kuvamiwa, lakini hakuna yanayohusisha
kiongozi wa CCM, badala yake ni raia wa kawaida na viongozi wa dini na
siasa. Nassari alidai akiwa kama wakala mkuu wa Chadema katika kata
hiyo, alikumbana na mambo kadhaa yaliyomshangaza, ikiwa ni pamoja na
kufanyiwa jaribio la kutekwa mara mbili, kabla ya kushambuliwa kwa
kipigo.
Alisema
pia anashukuru kwamba askari wawili waliokuwepo katika eneo hilo
walijitahidi kutaka kumnusuru, lakini walizidiwa nguvu na vijana hao,
hasa kutokana na kutokuwa na bunduki, ambapo yeye alipofanikiwa
kuchoropoka alikimbilia bastola yake na kuwanyoshea vijana hao bila
kufyatua.
Akizungumzia
kuhusu hali yake, Nassari alisema amepimwa kipimo cha X-ray ambapo
imeonyesha kuwa pingili za mgongo wake zipo sawa, lakini daktari
ameshauri afanyiwe kipimo kingine kiitwacho MRI ili kuangalia hali ya
mishipa kutokana na maumivu makali anayoendelea kuyapata.
Aidha
alitumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge wa Kuteuliwa, Joseph Mbatia kuwa
ndiye aliyemsaidia kufanya mipango kuwasiliana na uongozi wa Bunge na
kumwezesha kuhamishiwa Moi, baada ya wabunge wote wa Chadema kwenda
Arusha kushughulikia waliofariki kwa bomu.
Hata
hivyo, Lowassa alipotafutwa kuhusiana na tuhuma hizo alikataa
kuzungumzia suala hilo na kusema hilo aulizwe Msimamizi wa Uchaguzi,
Paulo Kitaleki.
Mwananchi
ilimtafuta Kitaleki ambaye pia ni katibu tarafa, alikanusha kuhusika
kwa Lowassa akielezea kuwa siku ya tukio hilo alikuwa Geita.
“Huyu
Nassari ni mwigizaji na anafaa kuwa msanii kwa kuwa anaigiza tu hata
hakupigwa, bali yeye ndiyo aliyempiga Wakala wa CCM, Hussein Osama
ambaye ni mlemavu, kisha akatimua mbio baada ya vijana kutaka
kumkamata, nashangaa kumwona yupo hospitali akidai kupigwa, siyo
kweli,” alisema Kitaleki.
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment