Meya wa Mji Mkuu wa Kampala nchini Uganda akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhumza za kusababisha vurugu.
Kampala, Uganda. Watu wawili wameuawa kwa risasi nchini Uganda juzi, wakiwa katika mkusanyiko kwenye eneo la soko la Kisekka.
Meya wa mji mkuu wa Uganda, Kampala, Erias Lukwago, pia alizirai baada ya kupigwa na polisi hao waliofyatua risasi za mipira kuutawanya umati wa wafuasi wake.
Akiwa kitandani, Meya huyo amesema baada ya kupata kipigo hicho alipoteza fahamu na kukimbizwa hospitalini.
“Bomu ambalo lilinifanya nipoteze fahamu lilirushwa katika gari langu na kuingia ndani,” amesema.
Meya huyo ni mpinzani wa rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, alieleza kwamba maofisa wa polisi walimpiga kifuani na kuzirarua nguo zake wakimtuhumu kwa kuchochea ghasia.
Katika tukio hilo, imedaiwa kwamba mtu mmoja anadaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kukamatwa wakati wa ghasia hizo.
Hata hivyo, polisi wamekanusha madai ya kumpiga meya huyo, ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Rais Museveni.
Upinzani umesema kuwa serikali inajaribu kukandamiza kilio cha mageuzi nchini humo.
Katika tukio lingine, kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye alikamatwa kwa kuandaa mkutano ambao polisi hawakuuidhinisha.
Lukwago, juzi alikuwa anaelekea kwenye jopo maalumu kwa mara ya kwanza, ambako huenda ikamwondolea wadhifa wake kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Polisi walizingira nyumba yake na kisha kumpeleka ambako jopo lilikuwa linaendesha vikao vyake.
“Walinipiga kifuani na kudai kuwa nachochea ghasia, walinirarulia nguzo zangu na kunitesa, nilijaribu kuwaambia waniache lakini sikufanikiwa,’’ amesema Lukwago.
No comments:
Post a Comment