Monday, April 22, 2013

Liewig akabidhi majina ya anaowabakiza Simba.

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikielekea ukingoni, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, tayari ametoa mapendekezo ya wachezaji watakaobaki Msimbazi.
Kocha huyo alijiunga na klabu hiyo katikati ya msimu huu akichukua mikoba ya Mserbia, Milovan Cirkovic, aliyetimuliwa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga, alisema wachezaji wengi waliopendekezwa na Liewig ni vijana.
 
“Ni mapema kuzungumzia usajili katika kipindi hiki, lakini kikubwa ni kwamba kocha tayari amekabidhi orodha ya wachezaji anaowahitaji watakaoendelea kuichezea Simba katika msimu ujao.
“Wachezaji hao aliowapendekeza wengi wao ni vijana tuliowapandisha msimu huu na wachache wa timu ya wakubwa ambao amepanga kuwaandaa zaidi,” alisema Kamwaga.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...