Monday, April 22, 2013

Mpango wa bunge kuidhinisha Sheria ya ndoa za jinsia moja Ufaransa wazua kizazaa mjini Paris.

Siku mbili kabla ya bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria inayohalalisha ndoa za jinsia moja kumetokea maandamano ya dakika za mwisho mwisho mjini Paris.
Watu wanaopinga sheria hiyo wamekusanyika katika eneo la Montparnasse la mji mkuu katika juhudi za mwisho za kuizuia sheria hiyo, huku maandamano mengine ya kundi hasimu pia yaliandaliwa kuiunga mkono sheria hiyo.
 Zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita katika maandamano mengine ya kupinga ndoa za jinsia moja.
Makundi ya kutetea haki za binadamu pia yameripoti ongezeko la matusi na mashambulizi ya kimwili dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji nchini Ufaransa.
Ufaransa inatarajiwa kuwa nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za jinsia moja, kufuatia kuidhinishwa sheria hiyo nchini New Zealand wiki iliyopita.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...