Monday, April 22, 2013

TAPELI ANAYETUMIA JINA LA WAZIRI LUKUVI AMTAPELI LOWASSA IRINGA

maofisa  wa  polisi mkoa wa  Iringa
wakiweka mtego katika nje ya
 ukumbi wa St Dominic  ili kumnasa
  tapeli  huyo anayejiita ni mtoto  wa
  waziri Lukuvi  na kutapeli  watu
Tapeli  anayetapeli  watu maeneo
 mbali mbali ya Tanzania  kupitia jina
 la  waziri Lukuvi akiingizwa ktk  gari maalum leo
Tapeli  Jonathan Wiliam Lukuvi
feki akitiwa matatani askari kanzu  Iringa
Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dkt
 Christina  Ishengoma ,askofu Dkt
Boaz Sollo na Waziri mkuu wa
  zamani Edward  Lowassa akimsikiliza
 tapeli huyo akimpa maneno ya kitapeli  Lowassa
Kijana  huyo Tapeli akimsomesha
waziri Lowassa ukumbini kwa
kuahidi kuchangia 100,000 huku
akimwomba  kumsaidia misaada  zaidi
Hapa akipelekwa  katika gari
 maalum Hapa akiingizwa katika
Taxi tayari  kwenda  polisi
Kijana ambae amekuwa akiwaliza
 watumishi mbali mbali wa umma na watu
 binafsi  kwa  kutumia jina la waziri wa nchi
  ofisi ya  waziri mkuu  sera na uratibu
 wa bunge kijana Jonathan
Wiliam Lukuvi( si jina lake halisi)
amekamatwa katika hafla ya kanisa la
Overcomers FM akitaka  kumtapeli  waziri mkuu  wa zamani  Edward Lowassa kupitia harambee  hiyo.
Kijana  huyo  aliingia katika ukumbi
wa  St.DOminic leo  katika harambee ambayo mgeni  rasmi  alikuwa ni Lowassa na  kupita mbele
 na kutumia kipaza  sauti  kuzungumza
kuwa anaitwa  JOnathan Wiliam Lukuvi
 na ni mtoto  wa  waziri wa nchi  ofisi
 ya  waziri mkuu sera na uratibu  wa
 bunge na kuwa amekuwa akimpigia
 simu mara kwa mara  Lowassa na hata
 katika mkutano  wake
 wa Jangwani  jijini Dar es Salaam
alipata  kuzungumza na Lowassa na  hivyo kuomba  kutekelezewa  ombi lake la msaada ambao hakuutaja.
Kutokana na  utambulisho  huo
  baadhi ya  watu  waliopata  kutapeliwa
na kijana  huyo akiwemo mkurugenzi
  wa Halmashauri ya Manispaa ya
 Iringa  waliweza kuguna hali iliyopelekea  askari  polisi  kufunguka na kumtia mbaroni
kijana  huyo ambae alikuwa akiweka mtego  wa kumtapeli  Lowassa  na  viongozi
 wengine katika hafla  hiyo .
Hata  hivyo  baada ya  polisi  kumtia
 nguvuni kijana  huyo  baadhi ya  watu
waliotapeliwa  waliweza  kumtambua
 huku familia ya  Lukuvi iliyokuwemo
 katika ukumbi  huo  ikimkana katu katu
kuwa hana hata  chembe ya familia na
watu hawamtambui .
Kada  wa CCM maarufu mkoani Iringa
 Godfrey  Malenga  Lukuvi  alisema
  kuwa  kijana  huyo  amekuwa akitumia
jina la waziri Lukuvi  kuliza  watu na
 kuwa wengi  wamekuwa  wakilalamika
 kuhusu  utapeli  unaofanywa na kijan
a  huyo na kuwa tayari alipata
kukamatwa na  polisi ila alitolewa .

Kwa  upande  wake  katibu
wa mbunge  jimbo la Isimani ambae
 pia ni familia ya  Lukuvi Bw  Thom
Malenga  Lukuvi alisema  kuwa amekuwa
akipokea malalamiko mbali mbali kutoka
 kwa watu mbali mbali ambao
 wamelizwa na kijana  huyo na kuwa
 siku  zote  alikuwa akiweka mtego
ili kumnasa kijana  huyo
tapeli  japo hakufanikiwa  kumpata.

Thom ambae  yupo  nje ya mkoa
  wa Iringa  kwa shughuli za kifamilia
 alisema kuwa alitamani  sana kama
 angebahatika  kumshuhudia kwa
macho kijana  huyo tapeli
 ila kwa kuwa  yupo nje ya mkoa
atajitahidi  kurudi mapema mjini
 Iringa ili kumwona  tapeli huyo.

Kwa  upande  wake mkurugenzi
  wa Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa  Teresia Mahongo
 alimweleza mwandishi  wa mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com kuwa pia
kijana  huyo alipata  kufika  ofisini
kwake kwa ajili ya kumtapeli na baada ya
  kumshtukia alimtafuta  waziri
Lukuvi kwa simu na kuelezwa kuwa  kijana  huyo ni tapeli  mkubwa .

Hata  hivyo  mwanahabari
 Gerald Malekela  wa radio
Nuru  Fm alisema kuwa  kijana
  huyo alipata  kufika  studio  za
 radio  hiyo kwa ajili ya  kutapeli
uongozi kwa  kutumia jina  hilo
 na kufika  studi  za radio hiyo
 huku akiwa na barua inayosifia
watangazaji na kuomba  kusaidiwa
  zaidi kama mmoja kati ya  wasikilizaji .
 Mtandao huu ulipata nafasi ya
  kumtafuta  kwa  njia ya simu
waziri  Lukuvi ambae  mbali ya
kumkana kuwa hamtambui
 bado alisema  kuwa amepata
  kuwaliza  watu mbali mbali kwa  kutumia jina lake.

Lukuvi alisema kuwa tayari
  amepata kupokea malalamiko
kutoka kwa mkurugenzi wa
Manispaa ya Iringa na kumwagiza
 kumtakata na kutaka  sheria  ichukue mkondo  wake.

"Mimi  huyu  kijana  simtambui na
 wala  si ndugu yangu ila amekuwa
akitumia jina langu kutapeli  watu
 na tayari alikamatwa na polisi kwa  utapeli  huo"

Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Dkt
 Christina  Ishengoma aliwaonya
 watu  wanaoendelea  kutapeli
 wengine kwa  kutumia majina
 ya viongozi ama namna nyingine
  yeyote kuacha mara moja na kuwa
  akiwa kama mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama
 ya mkoa hatakubali kuona
matapeli hao  wakiendelea
  kulizwa  watu kwa njia ya udanganyifu .


Hata  hivyo aliwataka
wananchi  kujiepusha na wimbo
 hilo la utapeli kwa kuwaripoti
  polisi  watu  wanaowashukia kuwa ni matapeli .
Chanzo: Matukiodaima 

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...