Tuesday, March 27, 2018

MBOWE NA VIGOGO WENGINE WA CHADEMA WASWEKWA RUMANDE

Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wamefutiwa dhamana na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mbowe, viongozi wengien ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Viongozi hao wameripoti kituoni hapo leo Jumanne Machi 27, saa tatu asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kuitikia wito wa polisi ambao wamekuwa wakiwahoji kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali Februari 16, mwaka huu.
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredrick Kihwelo wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi ya viongozi walikuwa wanakaidi kuripoti polisi kila wanapotakiwa kufanya hivyo huku Msigwa akiongezwa katika orodha ya viongozi hao baada ya kuhojiwa jana na kupewa dhamana ambayo pia leo imefutwa.

“Baada ya kuhojiwa leo, wakaambiwa waendelee na mambo mengine wamepelekewa katika Ofisi ya Mpelelezi wakavuliwa viatu na mikanda, wakawekwa mahabusu.
“Walitakiwa kupelekwa mahakamani lakini bado kuna hali ya kusuasua lakini kwa mujibu wa ZCO, wameambiwa wamewekwa mahabusu kwa sababu wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi yao walikuwa wanakaidi wito wa polisi wakitakiwa kufika polisi, lakini hiyo si sababu ya msingi kwa sababu wangeweza kuwafutia wale ambao hawapo na si hawa wanaokuja kila siku,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, amesema ZCO amewaambia kesho watafikishwa mahakamanai lakini hadhani kwa sababu kuna mpango mbaya zaidi ila wanachokifanya leo ni kupeleka maombi Mahakama Kuu kuomba kesho wafikishwe mahakamani.
Walioshindwa kuripoti kituoni hapo Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kutokana na kufiwa na msiba huku Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akidaiwa kuwa nje ya nchi kwa matibabu.
Na Mtanzania.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...