Meneja wa TANESCO Mbeya akiongea na waandishi wa habari pembeni ni Kamanda wa polisi mkoani Mbeya DCP Mohammed Mpinga.
Polisi Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuwakamata watu wanne kwa tuhuma za kuingilia miundombinu ya shirika la umeme nchini (TANESCO).
Akiongea
na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi mkoani humo DCP Mohammed Mpinga
amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na maafisa wa Tanesco march 23, mwaka huu walifanya Oparesheni katika
maeneo ya vijiji vya Isebe na Isajilo vilivyopo Wilaya ya Rungwe kufuatia
taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanaingilia miundombinu ya Tanesco katika vijiji vyao pamoja na
kufanya wizi wa nguzo za umeme na kuwaunganishia umeme wakazi wa maeneo hayo
kinyume cha sheria.
Watuhumiwa wa uhujumu miundombinu ya TANESCO wakiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.
Amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni Idd Hamis Mwambusye Mkazi wa Bagamoyo, Benard Kibondi Mkazi
wa Kikota, Thobias Wilfred, Mkazi wa Iponjola, Eng. Geofrey Msunga Mkazi wa Mbeya.
Kamanda
Mpinga amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa
majumbani kwao walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme ikiwa ni pamoja na Mita
za umeme 27, nyanya za umeme mkubwa na ndogo, nguzo 57 za umeme ambazo walikuwa
zikitumika kuwaunganishia umeme wananchi pamoja na vifaa vingine.
Watuhumiwa
watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Pia ameelez kuwa
jeshi hilo litaendelea na msako mkali kuwasaka watuhumiwa wengine
wanaojihusisha na uhujumu wa miundombinu ya Shirika la Umeme TANESCO katika maeneo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment