Tuesday, March 27, 2018

MAAJABU: JENEZA LAKUTWA NJE YA GETI LA NYUMBA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nelson Edson mkazi wa eneo la Nsalaga Uyole Jiji la Mbeya amestaajabu baada ya kuamka na kukuta jeneza nje ya geti la nyumba yake lililowekwa na watu wasiojulikana.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa mtaa huo Paulo Ngonde amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia siku ya leo March 27, 2018 ambapo alipigiwa simu na mjumbe wa mtaa huo juu ya uwepo wa tukio la jeneza kukutwa nje ya nyumba ya Nelson Edson.
Aidha Mwenyekiti Ngonde ameongeza kuwa katika mtaa wake kumekuwa na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na matukio ya utupaji watoto lakini hili la kukutwa kwa jeneza nyumbani kwa mtu ni la kwanza.

Ameongeza kuwa baada ya kupata taarifa hizo walitoa taarifa kituo cha polisi cha Uyole pamoja na kwa wazee wa mila wa mtaa huo ambapo baada ya kufungua jeneza hilo wamekuta halina kitu ndani licha ya kufungwa kwa kitambaa (sanda) nyeupe.

Baadhi ya majirani wa mhanga wa tukio hilo wamesema wanashangazwa na tukio hilo ambalo hawajui lina kusudi gani kwani mhanga huyo ni mgeni katika eneo lao na kuongeza kuwa nyumba hiyo ni mpya na amehamia hivi karibuni.

Kamanda polisi mkoani Mbeya DCP Mohammed Mpinga amekiri kupata taarifa hiyo na kuahidi kulitolea taarifa rasmi baada ya uchunguzi kukamilika.

Na. YonnaMgaya

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...