Katika mchezo uliochezwa jana Mjini Madrid, Isco alifunga mabao matatu na kuwasaidia Uhispania kupata ushindi mnono wa 6-1 dhidi ya Argentina ambao walifika fainali Kombe la Dunia 2014.
Uhispania waliongoza 2-0 baada ya Diego Costa kumbwaga Sergio Romero kisha Isco akafunga bao lake la kwanza.
Argentina, waliomkosa Lionel Messi ambaye anauguza jeraha, walifanikiwa kufunga bao moja kupitia Ulled Nicolas Otamendi aliyefunga kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Isco na Thiago Alcantara kisha walifunga na kufanya mambo 4-1 kabla ya nguvu mpya Iago Aspas kuongeza bao la tano.
Isco alikamilisha ushindi wao wa kufunga bao la kukamilisha 'hat-trick' yake.
Uhispania ambao walishinda Kombe la Dunia 2010 sasa hawajashindwa mechi 18 tangu Julen Lopetegui alipochukua usukani baada yao kuondolewa mapema hatua ya muondoano EURO 2016.
No comments:
Post a Comment