Wednesday, March 28, 2018

TANESCO KUTUMIA MFUMO MPYA WA MALIPO YA SERIKALI KUUZA UMEME WA LUKU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).

Mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali. Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya TANESCO makao makuu imeeleza kuwa shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali, hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki. 

"Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.

" Baadhi ya taasisi hizo ni Polisi, Brella, Ardhi, TRA pamoja na Mamlaka za maji. Tunapenda kuwahakikishia wateja wote kuwa mbali na Kampuni za simu ofisi zote za Shirika na vituo vya mauzo ya LUKU vitaendelea kutoa huduma katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka,"imesema taarifa hiyo.

Ufafanuzi huo wa TANESCO unakuja baada ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadai mkataba kati ya Tanesco na Maxcom (MaxMalipo) wa kuuza token za umeme utakwisha mwisho mwa nwezi hui na hakuna dalili wataongezewa mkataba.

Taarifa hiyo ikadai kutokana na hali hiyo ni vema wateja wakachukua tahadhari kwani baada ya Machi 31 anayetaka kununua umeme itabidi aende ofisi za TANESCO.

Hivyo TANESCO wameamua kufafanua kuhusu mfumo mpya ambao utatumika wateja kununua umeme na kuwahakikishia wataendelea kununu kama zamani na hakutakuwa na tatizo lolote.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...