Thursday, May 29, 2014

HALIMA MDEE AMVURUGA WAZIRI TIBAIJUKA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka jana alijikuta katika wakati mgumu wakati alipokuwa waziri wa kwanza kuhusishwa na tuhuma za ufisadi wa kutumia vibaya madaraka yake na lawama lukuki kuhusu kasoro za kiutendaji katika wizara anayoiongoza.


Mawaziri wengine wamekuwa wakiwekwa kitimoto kutokana na tuhuma za utendaji mbovu na udhaifu kwenye wizara zao, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati Waziri Kivuli wa Ardhi, Halima Mdee aliposoma hotuba ya kurasa 77 ya upinzani kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huku kurasa 30 zikielekeza tuhuma kwa waziri huyo.
Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa dhidi ya waziri huyo ni pamoja na kujinufaisha kupitia mgogoro wa ardhi katika eneo la Chasimba na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill jijini Dar es Salaam.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alimhusisha waziri huyo na ufisadi katika kazi ya utafiti uliofanywa na wataalamu wa masuala ya ardhi, uliogharimu Sh700 milioni. Tuhuma hizo zilimchanganya Waziri Tibaijuka kiasi kwamba wakati akitoa majibu alijikuta akitoka nje ya mada na kumshambulia Mdee, huku Spika Anne Makinda akimrudisha kila mara na kumtaka ajikite kwenye hoja na kuacha kushambulia wapinzani.
Waziri Tibaijuka pia alidai hotuba ya upinzani ilijaa uongo na kumtaka Spika Makinda kumchukulia hatua Mdee. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Akisoma maoni ya Kambi ya Upinzani bungeni jana, Mdee alisema utafiti huo ulikuwa na timu ya watu 140 kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo, sekta binafsi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema waziri huyo anatuhumiwa kuingilia mchakato huo kwa kuingiza jamaa zake na taasisi ambazo ana uhusiano nazo kama sehemu ya kikosi kazi cha utafiti kwa jina la wataalamu washauri.
"Matokeo yake, Idara ya Uchumi ya UDSM ilitumika kama chambo huku kiasi kikubwa kikimrudia mwenyewe kwa mlango wa nyuma," alisema Mdee.
"Ilifika hatua wataalamu walimsusia kazi waziri kutokana na kuwepo ujanja ujanja katika masuala ya fedha, hivyo kumlazimu waziri kujifungia na wasaidizi wake kukamilisha kazi iliyobaki."
Kadhalika Mdee alimtuhumu Tibaijuka kwamba ana uhusiano na Taasisi ya Tanzania Women Land Access Trust (TAWLAT) ambayo ililipwa kiasi cha Sh300 milioni kutoka Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kutoa elimu na kuendesha mazungumzo kwa diplomasia, kati ya viongozi na wananchi wa Chasimba kuhusu mgogoro wa ardhi.
"Licha ya kulipwa fedha hizo, TAWLAT haikufanya kazi yoyote ya uthamini katika eneo la Chasimba, badala yake aliyekuwa mkurugenzi wa upimaji, mthamini mkuu wa serikali pamoja na wataalamu wa wizara walikuja kuniomba niwatulize wananchi waliokuwa wanawarushia mawe kwa kuwa hawakuwa na imani na viongozi hao," alisema Mdee.
Mdee, ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema), aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuichunguza TAWLAT kuhusu ushiriki wake aliosema una shaka katika kazi kadhaa za Wizara ya Ardhi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
CHANZO:MWANANCHI

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...