Tuesday, May 27, 2014

NI TIMU NANE TU ZIMETWAA KOMBE LA DUNIA

Vijana wa Brazil  

London, England. Kwa kipindin cha miaka 83, fainali za Kombe la Dunia zimefanyika mara 19, lakini hadi sasa ni timu nane tu ambazo zimeshatwaa ubingwa wa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani.
Fainali hizo zilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1930 nchini Uruguay na zimekuwa zikifanyika kila baada ya miaka minne, isipokuwa mwaka 1942 na 1946 kutokana na Vita Kuu ya dunia .
Brazil inaongoza kwa kutwaa Kombe la Dunia baada ya kutwaa taji hilo mara tano. Brazil ilitwaa taji hilo nchini Sweden mwaka 1958, nchini Chile (1962), Mexico (1970), Marekani (1994) na Korea/Japan (2002). Brazil pia ndiyo nchi pekee iliyoshiriki fainali zote za Kombe la Dunia tangu zilipoanzishwa mwaka 1930 na imefunga jumla ya 210 katika fainali 19.
Italia imetwaa ubingwa huo mara nne. Ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza ilipoandaa mwaka 1934, baadaye nchini Ufaransa (1938), Hispania (1982) na Ujerumani (2006). Italia imeshiriki fainali hizo mara 17 na kufunga mabao 126. Kati ya 1950 na 1990, Ujerumani Magharibi (sasa Ujerumani) ilitwaa ubingwa mara tatu. Ilitwaa ubingwa nchini Uswisi 1954, na baadaye ilipoandaa fainali hizo mwaka 1974 na nchini Italia (1990). Kati ya 1930 mpaka 2010 Ujerumani imeshiriki fainali hizo mara 17 na imefunga mabao 206.
Mwaka 1978, Argentina ilikuwa ni taifa la tano kutwaa ubingwa wa dunia. Ilitwaa tena ubingwa wa dunia mwaka 1986. Tangu 1930 mpaka 2010, Argentina imeshiriki fainali hizo mara 15 na kufunga mabao 123.
Uruguay ilikuwa nchi ya kwanza kutwaa kombe hilo wakati ilipoandaa fainali hizo 1930. ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pilimwaka 1950 nchini Brazil. Uruguay imeshiriki Fainali za Kombe la Dunia mara 13 na kufunga mabao 76. Ufaransa imetwaa ubingwa wa dunia mara moja mwaka 1998 walipokuwa wenyeji. Ufaransa imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 13.
Pamoja na utajiri wa vipaji na kuwa na klabu bora, Hispania ilisubiri hadi mwaka 2010 kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza na ndio mabingwa watetezi. Hispania imeshiriki fainali hizo mara 13 na kufunga mabao 88.England iliandaa na kutwaa ubingwa mwaka 1966. Imeshiriki mara 13 na kufunga mabao 77. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...