MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela askari saba wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambao walikuwa wakishtakiwa kwa mauaji.
Akitoa
hukumu yake katika kikao cha Mahakama Kuu kilichokuwa kikifanyika
mkoani Kigoma Jaji wa mahakama hiyo, Sam Mpaya Rumanyika alisema kuwa
baada ya kupitia ushahidi mbalimbali Mahakama hiyo imewatia hatiani
askari hao kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Katika
kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012 washitakiwa hao walifikishwa
mahakamani hapo na kusomewa shitaka la kumuua Festo Stephano, mkulima wa
kijiji cha Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu mkoani hapa katika tukio
lililotokea Agosti 6, mwaka 2011.
Askari
hao waliohukumiwa ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo
Swahib, D/C Charles, D/C Shamsi, D/C Jerry na D/C Amrani ambao kwa
pamoja walikana shitaka lao katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012.
Akitoa
utetezi kabla ya hukumu hiyo wakili wa washitakiwa, Method Kabuguzi
aliiomba Mahakama kuwafutia shitaka washitakiwa hao na kuwaachia huru
kwani wote bado vijana na wameoa hivi karibuni.
Sambamba
na hilo Kabuguzi alisema kuwa askari hao walikumbwa na mkasa huo wakati
wakitekeleza jukumu lao la ulinzi wa taifa ambapo walimkamata mtuhumiwa
wa kutumia silaha na ndipo kifo kikatokea wakati wakitekeleza majukumu
yao.
No comments:
Post a Comment