Thursday, May 22, 2014

YAYA AITIA KIWEWE MANCHESTER CITY

Yaya Toure amekoleza moto kwenye sakata lake kutaka kuihama Manchester City akisema hajui hadi sasa atakapokwenda kucheza msimu ujao.
Wakala wa mchezaji huyo, Dimitri Seluk alibainisha kuwa Yaya anaweza kuondoka kwa sababu anadhani kwamba amekuwa akichukuliwa kama mtu asiyeheshimika na wamiliki wa klabu hiyo.
Hivyo kwa sasa, Toure ambaye ana miaka 31, hajaamua hatima yake kuhusu klabu atakayochezea msimu ujao.
Alipoulizwa kama anaweza kuichezea klabu nyingine msimu ujao, alijibu: “Ndio. Hatujui katika soka nini kitatokea. Kamwe hatuwezi kujua hilo.”
Katika mahojiano maalumu na mtandao wa BE IN SPORTS, nyota huyo wa timu ya taifa ya Ivory Coast alisema: “Kwa sababu ya msimu mzuri niliokuwanao klabu ya Man City, kila mtu ananizungumzia na kila kitu kiko wazi.
“Wakala wangu Dimitri, siku zote amekuwa akizungumza na watu kwa simu na anajua cha kufanya kwa sababu siku zote nimekuwa nikimuamini sana.
“Hatujui kesho itakuwaje, lakini kwa sasa akili yangu iko katika Kombe la Dunia na baada ya kumalizika kwake tutajua nini kimetokea.”
Toure alisaini mkataba mpya wa miaka minne kuichezezea City Aprili mwaka jana.
Hata hivyo, majaaliwa yake yamebaki kuwa na mashaka kutokana na wakala wake kuwalaumu wamiliki wa City kwa kutoonyesha heshima kwa kiungo huyo alipotimiza miaka 31. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...