Raheem Sterling
Klabu
ya Manchester City ya Uingereza imekubaliana na wapinzani wao Liverpool
dau la pauni milioni £49 kumsajili mshambulizi Raheem Sterling.
Uhamisho wa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa unategemea makubaliano baina yao na vipimo vya afya. Sterling alikuwa ameomba kundoka Anfield kabla ya klabu hiyo kukataa dau mbili za Man City mwezi Juni.
Mshambulizi huyo atakuwa
mchezaji aliyegharimu pesa nyingi zaidi raia wa Uingereza baada yake
kukatalia mbali mshahara wa pauni laki moja kwa juma kutoka Liverpool.
Sterling aliyejiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka 15 kutoka
QPR mwezi februari mwaka wa 2010 yuko katika kandarasi inayokamilika
mwaka wa 2017. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
QPR inatarajiwa kupokea asilimia 20% ya ada ya kukuza kipaji chake kutoka kwa pesa hizo.
Jumamosi
iliyopita ,Sterling alikuwa ametajwa katika kikosi kitakachozuru
Thailand, Australia na Malaysia, lakini jina lake likaondolewa.
Wachezaji kadha wakongwe wa
klabu hiyo wamemkashifu kwa kutaka kuihama klabu hiyo tangu kocha
Brendan Rodgers na mkurugenzi mkuu Ian Ayre kutangaza kuwa alikuwa na
nia ya kuihama.
Hivi majuzi utafiti ulimorodhesha kama mchezaji mwenye thamani zaidi barani ulaya.
Mchezaji wa Paris St-Germain Marquinhos alikuwa wapili huku Memphis Depay aliyeihamia Manchester United akiorodheshwa tatu bora. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
Mchezaji wa Paris St-Germain Marquinhos alikuwa wapili huku Memphis Depay aliyeihamia Manchester United akiorodheshwa tatu bora. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
No comments:
Post a Comment