Monday, July 13, 2015

POLISI WANNE WAUAWA KATIKA SHAMBULIO

Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo
Maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania.

Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam. Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.

Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Kwa mujibu na raia wanoishi karibu na kituo hicho,makabiliano ya risasi yalidumu kwa zaidi ya saa moja.
Uchunguzi unaendelea kujua nani aliyetekeleza shambulizi hilo
Mkuu wa polisi Ernest Mangu amethibitisha uvamizi huo akisema askari 4 na raia 3 wameaga dunia. Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.

Aidha amesema kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...