Wednesday, May 13, 2015

NGASSA ASAINI KUCHEZA AFRIKA KUSINI

Mrisho Ngassa

 Mshambuliaji hodari wa timu ya Yanga, Mrisho Ngassa amemwaga wino wa kuichezea timu ya Free State Stars ya ligi kuu Afrika Kusini kwa miaka minne.

 Ngassa ameripotiwa kufurahia mkataba huo mnono na kuanza maisha yake mapya baada ya kucheza nyumbani kwa miaka kadhaa.

"Nataka kuitumia fursa hii kutangaza soka la Tanzania na nitajituma ili kufanya vizuri zaidi" alisema mchezaji huyo.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii Ngassa ameonekana akiwa na kocha wa timu hiyo mara baada ya kusaini mkataba.


No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...