Wednesday, January 07, 2015

"KIWANGO CHA NGASSA KIMESHUKA, LAKINI NI MCHEZAJI MWENYE AKILI, LAZIMA ATARUDI KATIKA KIWANGO CHAKE" - PLUIJM

KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm anaamini Mrisho Ngassa atarudi katika kiwango chake cha zamani.
Pluijm alikiri wazi kuwa nyota huyo ameshuka kiwango kwa sasa  na ndio maana anaanzia benchi katika mechi mbalimbali, lakini anaonesha juhudi kubwa mazoezini kitendo kinachoonesha wazi ametambua alipo sasa.
“Kiwango cha Ngassa kimeshuka, lakini ni mchezaji mwenye akili, lazima atarudi katika kiwango chake”. Alisema Pluijm.
NGASSA-MRISHO
Kocha huyo anayependa soka la kushambulia aliongeza kuwa kwasasa kikosi chake kimesheheni nyota wa kiwango cha juu, hivyo inawalazimu wachezaji kufanya jitihada za kumshawishi.
Moja kati ya mechi kubwa ambayo Ngassa hakuanza chini ya Pluijm mwishoni mwa mwaka jana ni ile ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam fc iliyopigwa desemba 28 mwaka jana uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Ngassa alichezeshwa dakika 7 tu kitendo kilishoashiria mchezaji huyo kipenzi kwa Wana Yanga si mchezaji tegemeo tena katika kikosi cha Yanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kocha huyo aliongeza kuwa siku zote anapenda kucheza mpira wa wazi, akishambulia zaidi kwa lengo la kufunga magoli mengi, hivyo nguvu zake zipo katika kuwanoa viongo wake na washambuliaji wake.
Kwasasa Pulijm anapenda kuwatumia zaidi Kpah Sherman, Danny Mrwanda, Amissi Tambwe, Saimon Msuva, Andrey Coutinho katika safu ya ushambuliaji, huku Ngassa, Hussein Javu wakianzia benchi.
End…………
MOJA ya vitu anavyopenda kocha mpya wa Simba, Goran Kopunovic ni kuzingatia muda, nidhamu, kujituma na heshima.
Wachezaji wengi wa kitanzania wamekuwa na matatizo katika mambo hayo anayopenda kocha huyo raia wa Serbia hasa kutozingatia muda.
Kopunovic katika programu zake za mazoezi hataki hata kupoteza dakika moja.
Meneja wa Simba, Nico Nyagawa amekiri kuwepo kwa mabadiliko katika kikosi chao hasa suala la muda.
“Ni kocha anayezingatia sana muda, hataki kupoteza hata dakika moja. Hili ni jambo muhimu sana kwasababu wachezaji wengi wa Kitanzania wana tatizo la kutofuata muda”. Alisema Nyagawa.
End……….
ROBO fainali ya kwanza ya kombe la Mapinduzi inapigwa leo majira ya saa 2:15 usiku uwanja wa Amaan Zanzibar baina ya Simba na Taifa ya Jang’ombe.
Mechi hii imetabiriwa kuwa tamu kutokana na kiwango kikubwa walichoonesha Simba katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya JKU ambapo walishinda goli 1-0.
Siku hiyo Simba waliuanza mchezo kwa kasi katika vipindi vyote, wakicheza pasi za haraka haraka na kutumia njia ya pembeni kuipenya ngome ya JKU.
Kocha Goran Kopunovic alitumia muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake namna ya kucheza mpira ambapo alisisitiza kwa ishara akiwataka wachezaji wapigiane pasi na kushambulia kupitia mawinga na kukaba kwa uangalifu.
Kocha huyo ameonekana kupenda kucheza mpira wa kasi muda wote na amekuwa akiwapa wachezaji wake mazoezi magumu ya kuongeza nguvu na pumzi.
Robo fainali nyingine tatu zitapigwa kesho uwanja wa Amaan ambapo majira ya saa 9:00 alasiri, mabingwa watetezi, KCC ya Uganda watachuana na Polisi Zanzibar.
Azam fc watashuka dimbani katika robo fainali ya tatu majira ya saa 11:00 jioni kuonesha kazi na Mtibwa Sugar.
Hii itakuwa mechi kali kutokana na ubora wa timu zote hususani Mtibwa Sugar wanaoongoza katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Robo fainali ya mwisho itawakutanisha Yanga na JKU majira ya saa 2:00 usiku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...