IPO misemo mingi ambayo huashiria
kutokea kwa jambo liwe nzuri au baya, moja ya misemo hiyo ni ule usemao
dalili ya mvua ni mawingu.
Msemo huu unaweza ukawa na na
maana kubwa hivi sasa kwa golikipa wa timu ya Dar es salaam Young
African, Juma Kaseja ambaye hivi sasa inaonekana hana mawasiliano mazuri
na uongozi wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani
jijini Dar es salaam.
Mchezaji huyo mwenye heshima
kubwa nchini mwishoni mwa mwaka uliopita aliachwa katika kikosi cha timu
hiyo kilichoelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya mapinduzi,
lakini isitoshe jina la Kaseja halijaonekana kwenye orodha ya wachezaji
wa timu hiyo iliyotumwa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa ajili
ya ushiriki wa kombe la shirikisho.
Matukio hayo yote yameibua
maswali mengi kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo juu ya hatma ya
mlinda mlango huyo, hatua iliyotufanya tumtafute afisa habari na
mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro kutaka kufahamu kinaga ubaga
kinachoendelea kati ya Kaseja na Yanga..
Muro amesema Kaseja kutohusishwa katika kikosi kilichopo Zanzibar na kilichotumwa CAF ni kujitakia mwenyewe.
Jerry Muro.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Ni vizuri tukianza kuwakumbusha
wapenzi wetu tulipotoka tulipo na tunapoelekea na mimi nilipoingia
nililikuta hili tatizo lipo na tulipoamua kulifuatilia na kulipatia
ufumbuzi, lazima tuseme ukweli na kweli itatuweka huru, matatizo ya Juma
Kaseja na Yanga yalisababishwa na yeye mwenyewe alipoona hana
kipaumbele na Yanga”.
Na hii ilitokana na kutokupangwa
mara kwa mara katika michezo mingi ya Yanga tofauti na zamani watu
walivyokua wakimuelewa kama kipa bora Tanzania, lakini kwa mabadiliko
ambayo klabu imekua ikipitia kwa namna moja na kwa mahitaji ya timu
labda yalikua hayamfurahishi Juma kama binadamu’’ alisema.
Muro ameendelea kusema kwamba
“ndani ya uongozi wa yanga benchi la ufundi liliamua kumtumia Dida
kutokana na uwezo wake jambo ambalo Juma hakupata nafasi kutokana na
mahitaji ya timu hali iliyopelekea baadhi ya mashabiki kulalamika kwa
nini hapangwi”
“Lakini tuweke kumbukumbu zetu
vizuri Kaseja kapangwa mechi ya Mtibwa kafungwa magoli mawili,
kachezeshwa mechi dhidi ya CDA ya kirafiki na nyingine kule Shinyanga,
pia ikumbukwe wakati Juma yupo Simba na hata na Yanga alikuwa anapangwa
michezo yote hadi ya kirafiki, mbona wenzake hawakulalamika hadi kuamua
kuondoka?
“ Lakini kwanini watu wanahoji
kipindi hiki ambacho klabu imeamua kuinua vipaji na kutafuta watu
wengine wa kuchukua nafasi ya Juma …? Aliuliza Muro, na kuongeza huo
ndio mgogoro na Juma na sio wa maslahi…
Kuhusiana na kutoonekana
mazoezini Muro amesema juma alipoona hapewi nafasi akaamua mwenyewe
kuacha kuhudhuria mazoezi na tatizo hili lilianza taratibu.
“Ghafla Juma akasema haji
mazoezini kwa sababu anaidai Yanga mara akageuka akaandika barua akasema
hana matatizo na Yanga, mara mwanasheria wake akatuandikia barua ya
masuala ya kisheria”
Hata hivyo, Muro amesema kuhusu
ni lini Juma hajafika mazoezini aulizwe mwenyewe lakini kama hafanyi
kazi hakuna atakacholipwa na wanataratibu zao.
“Hata kama una mkataba haufanyi
mazoezi haulipwi na hili hatupepesi macho kama hatuna taarifa zako
kutoka kwa mwalimu au daktari wa timu hatujui kuhusu mambo yako ya
familia huji mazoezi hulipwi chochote na hatulipi chochote”.
Huo ni upande wa Yanga ambayo
bado ina mkataba na Kaseja, mchezaji mwenyewe anasemaje! Juhudi za
kumtafuta Juma Kaseja zinaendelea. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment