Ridhiwani
akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara
ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuwashuru kwa
kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya
wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa
ardhi.
Mkazi
wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani
Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
Mkazi
wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x
zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo
alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo
kusababisha kukosa maendeleo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
Mama
mwenye Jamii ya Kimasai Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge
kitendo cha baadhi ya wananchi kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya
wafugaji wanaofanya vurugu kwa kupeleka mifugo kwenye mashamba ya
wakulima na kuchafua visima vya maji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment