Bei ya mafuta ya
petroli, dizeli na ya taa nchini inazidi kushuka kutokana na kuporomoka
kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia tangu Juni mwaka jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati
na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alisema jana kuwa bei ya rejareja ya
petroli kuanzia leo imeshuka kwa Sh74, dizeli kwa Sh62 na mafuta ya taa
kwa Sh54.
Bei hizo zinashuka wakati kukiwa na mjadala mkali
kuwa bei zilizopo sasa hazisadifu hali halisi ya kuporomoka kwa mafuta
ghafi yanayouzwa kwa Dola 50 za Marekani kwa pipa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Ngamlagosi alisema bei hizo mpya zimekokotolewa kutokana na bei ya mafuta ghafi na kwamba huenda ikapungua zaidi siku zijazo.
Alisema kwa sasa bei ya jumla za nishati hiyo
zimepungua ukilinganisha na mwezi uliopita, kwani kwa lita petroli
imepungua kwa Sh73.75, dizeli Sh62.08 na mafuta ya taa kwa Sh54.34.
“Be za mafuta safi ya petroli kwa tani katika soko
la dunia imepungua kwa Dola 249 za Marekani, dizeli kwa Dola 189 na
mafuta ya taa kwa Dola 180.
Kufuatia bei hizo mpya, petroli katika vituo vya Dar es Salaam haitazidi Sh1, 955, dizeli Sh1,846 na mafuta ya taa Sh1,833.
Kutokana na gharama kubwa za usafirishaji, wakazi
wa Kyerwa Kagera ndiyo watakaokuwa wakinunua petroli kwa bei ya juu
zaidi kwa Sh2,192, dizeli Sh2, 083 na mafuta ya taa Sh2,070.
Ngamlagosi alisema ni vigumu bei iliyopo ikaendana
na bei ya sasa katika soko la dunia kwa kuwa mafuta yanayoingia nchini
hununuliwa kwa bei ya mwezi mmoja uliopita na kwamba kushuka kwa thamani
ya Shilingi kumechangia pia.
“Watu wanatakiwa wafahamu kuwa gharama za kodi
hazibadiliki. Pia kuna malipo ya usafirishaji na usambazaji, vyote
vinachangia karibu asilimia 40 ya gharama za mafuta.
“Asilimia 60 tu ndiyo inayoathirika na kushuka au kupanda kwa bei ya mafuta ghafi katika soko la dunia,” alisema.
Mhadhiri wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDBS), Dk Goodluck Urassa alisema bei hizo mpya
zinaendana na hali halisi ya soko la dunia.
Alisema huenda bei hizo zikapungua zaidi na kuimarisha bei ya bidhaa nyingine siku zijazo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisema bei ya mafuta ghafi imeshuka hadi
chini ya Dola 50, hivyo wito wake kwa Ewura ni kuweka wazi mfumo wa
kukokotoa bei za mafuta ili wachambuzi waone bei hizo ni halisi.
“Kwa hesabu zangu bei ingeshuka kwa angalau
asilimia 15 ya bei za sasa inayouzwa,” alisema Kabwe na kusisitiza
kuwapo uwazi katika kanuni ya kukokotoa bei za mafuta.
“Uwazi ndio suluhishi la ufisadi. Wananchi lazima wafaidike na punguzo la bei ya mafuta duniani,” alisema Kabwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Mwananchi
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment