Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi,
hivi karibuni alilazimika kununua nyumba za majirani wanaoizunguka
nyumba huko Barcelona Hispania bila kupenda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka SportsGrid
ni kwamba majirani wa Messi
walikuwa wanazifanyia marekebisho nyumba zao, lakini kwa bahati mbaya
wakaishiwa na fedha katikati ya marekebisho hayo huko mjini
Castelldefels, Spain, hivyo wakamuomba kijana tajiri Messi azinunue
nyumba hizo zilizokuwa kwenye marekebisho na kwa utaratibu Messi
akakataa.
Baada ya ombi lao kukataliwa majirani
wakaamua kuanza kufanya vitimbi ili Messi aone kero na kuamua kununua
nyumba zao, walizikodisha nyumba zao na wapangaji wao wakawa watu wa
fujo wenye makelele muda wote na hatimaye vitimbi hivyo vikazidi kuwa
kero kwa Baba Thiago na familia yake. Mara ya kwanza Messi alienda
kuongea nao waache tabia hizo lakini hali haikubadilika hivyo akaamua
kujenga ukuta mrefu wa kuitenganisha nyumba take na majirani - lakini
jaribio hilo likawa linaenda kinyume na baadhi ya sheria za Spain kuhusu
ujenzi na majirani wakatumia nafasi hiyo kutishia kumshtaki Messi.
Hivyo ili kuepeukana na skendo ya
kupelekwa mahakamani Messi akaamua kuwait a wanasheria wake na kuwaambia
wafanye taratibu za kisheria kufanya manunuzi ya nyumba zote za
majirani waliokuwa wakitaka kuziuza. Hatimaye mpango wa majirani
ukafanikiwa na Messi akanunua nyumba zote za majirani wake hivyo
kumfanya kuwa mmoja ya watu wanaomiliki maeneo makubwa kwenye sehemu
ya Castelldefels, Spain.
No comments:
Post a Comment