Thursday, April 18, 2013

AUNTY EZEKIEL: WABUNGE BAADA YA MATUSI BUNGENI SASA WANATAKA KUVUNJA AMRI YA 6!!


DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba
 kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake, 
Amani linasimulia aliyoyasema.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao 
wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na 
kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza 
kuhatarisha ndoa yake.

"Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini 
wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza:
 “Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na
 amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte,
 Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume
SOURCE: GPL

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...