Monday, June 24, 2013

MH. SUGU AMUOMBA RADHI WAZIRI MKUU

Mhe Sugu
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda
BAADA ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.

Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."

2 comments:

Unknown said...

Tumekusamehe kaka....tunajua zilikuwa hasira coz unamachungu xana na WATANZANIA

Unknown said...

tumekusamehe SUGU kwan tunajua zilikuwa ni hasira bcoz UNA MACHUNGU XANA MAISHA WANAYO ISHI WATANZANIA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...