Monday, June 24, 2013

SIKU 17 KABURINI... FAMILIA YASHANGAA RIPOTI KIFO CHA NGWEA.


ZIKIWA zimekatika siku 17 tangu aliyekuwa mkali wa Hip Hipo Bongo, Albert Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ alale kaburini, familia imeshangaa kupelekewa vitu vingine bila ripoti ya kifo chake.

Kwa mujibu wa mtu wa ndani wa familia hiyo, Millard Ayo wa Clouds FM ndiye aliyepewa majukumu ya kushughulikia kila kitu baada ya kifo tata cha Ngwea kilichotokea Johannesburg, Afrika Kusini Mei 28, mwaka huu.
 
Chanzo hicho kilieleza kuwa mara baada ya mwili wa marehemu Ngwea kuletwa Bongo, familia ilitarajia kukabidhiwa kila kitu ikiwemo ripoti ya nini kilimuua Ngwea.
 
“Hakuna swali tunaloulizwa kama ripoti ya kifo cha Albert (Ngwea). Kila mtu anataka kujua nini hasa kilitokea hadi akafa kwa sababu maneno ni mengi sana.
“Ripoti ndiyo ingeweza kumaliza maneno na kuwafunga watu midomo,” kilisema chanzo chetu mjini hapa.

Kiliendelea kunyetisha kuwa mwili ulipofika ilibidi familia ‘idili’ na maziko kwanza ambapo Millard aliahidi kuipeleka baada ya msiba.

“Kweli Millard alikuja tena juzikati, alichokabidhi ni cheti cha kifo (death certificate) na hati ya kusafiria ya marehemu Ngwea,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Familia nzima ilishangaa kwani ilikuwa ni tofauti na tulichotarajia lakini tulipomuuliza kuhusu ripoti ya kifo cha Ngwea, alikabidhi barua iliyoelezea kuwa chanzo cha kifo bado kinachunguzwa huko Afrika Kusini ambapo wanafanya critical investigation (uchunguzi wa kina) na tutajulishwa mara tu uchunguzi huo utakapokamilika.”

Baada ya kudakishwa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na mama wa marehemu Ngwea, Denisia Mangweha ambaye alikiri kupokea vitu hivyo na kwamba ni kweli familia ilijiandaa kupokea ripoti ya kifo lakini haikuwa hivyo.
Credit: GLP

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...