ROBO fainali ya kwanza ya kombe
la Mapinduzi inapigwa leo majira ya saa 2:15 usiku uwanja wa Amaan
Zanzibar baina ya Simba na Taifa ya Jang’ombe.
Mechi hii imetabiriwa kuwa tamu
kutokana na kiwango kikubwa walichoonesha Simba katika mechi ya mwisho
ya makundi dhidi ya JKU ambapo walishinda goli 1-0.
Siku hiyo Simba waliuanza mchezo
kwa kasi katika vipindi vyote, wakicheza pasi za haraka haraka na
kutumia njia ya pembeni kuipenya ngome ya JKU.
Kocha Goran Kopunovic alitumia
muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake namna ya kucheza mpira ambapo
alisisitiza kwa ishara akiwataka wachezaji wapigiane pasi na kushambulia
kupitia mawinga na kukaba kwa uangalifu.
Kocha huyo ameonekana kupenda
kucheza mpira wa kasi muda wote na amekuwa akiwapa wachezaji wake
mazoezi magumu ya kuongeza nguvu na pumzi.
Robo fainali nyingine tatu
zitapigwa kesho uwanja wa Amaan ambapo majira ya saa 9:00 alasiri,
mabingwa watetezi, KCC ya Uganda watachuana na Polisi Zanzibar.
Azam fc watashuka dimbani katika robo fainali ya tatu majira ya saa 11:00 jioni kuonesha kazi na Mtibwa Sugar.
Hii itakuwa mechi kali kutokana
na ubora wa timu zote hususani Mtibwa Sugar wanaoongoza katika msimamo
wa ligi kuu Tanzania bara.
Robo fainali ya mwisho itawakutanisha Yanga na JKU majira ya saa 2:00 usiku. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment