Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga akisindikizwa na Polisi kutoka katika Ukumbi wa Arnautoglu Dar es Salaam jana, baada ya mafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kumzonga alipokwenda kuhudhuria hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.
Wakati utata
ukizidi kujitokeza katika uapishaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa
Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na waliodaiwa kushinda kuwekwa kando na
kuapishwa walioshindwa, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro
Mahanga jana alikumbana na zomeazomea hadi kulazimika kuondoka kwenye
Ofisi za Manispaa ya Ilala, Arnatouglou ambako shughuli hiyo ilikuwa
ikifanyika.
Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM),
alizomewa akitakiwa kuondoka katika eneo hilo, akidaiwa kwamba
angebadilisha matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa chama chake.
Eneo hilo lilijaa wafuasi wa Chadema, CUF na CCM
huku kila kundi likiwa limesindikiza wenyeviti wake kuapishwa katika
shughuli ambayo ilifanyika kwa awamu tatu kwa kila jimbo; Segerea, Ilala
na Ukonga kupewa saa mbili.
Waziri Mahanga aliwasili wakati wa zamu ya Segerea
saa saba mchana, ndipo kundi la mashabiki wa upinzani lilipoanza
kumzomea na kuimba nyimbo za kumkashifu na kutaka atoke katika ukumbi
ulioandaliwa kwa ajili ya kuwaapisha wenyeviti. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Escrow... escrow... ondoka, hatukutaki. Hapa
hakieleweki mpaka uondoke, hatutaki uchakachuaji wako...” zilisikika
sauti za watu mbalimbali huku zikiimba nyimbo mbalimbali kumfukuza
mbunge huyo ukumbini.
Baada ya dakika takriban 25 za kelele hizo, waziri
huyo alinyanyuka na kuondoka huku wananchi hao wakimsindikiza kwa
nyimbo hizohizo na polisi wakifanya kazi yao ya kuhakikisha hadhuriki.
Wakati akiondoka, Dk Mahanga alikisogelea kikundi
kimoja kilichokuwa kinahoji alichokuwa amefuata wakati shughuli ya
uapishaji wenyeviti haimhusu na kujibu: “Wenyeviti wangu 59 wa Jimbo la
Segerea wanaapishwa leo. Kwa nini nisihudhurie? Kelele hizi zinaonyesha
jinsi gani ninavyotikisa jiji la Dar es Salaam.”
Baadaye akionekana mwenye kujiamini, mbunge huyo
alikatisha katikati ya kundi la mashabiki waliokuwa wakimzomea na
kuingia katika gari lake na kuondoka.
Kelele ziliendelea hadi gari la kiongozi huyo lilipotoweka kabisa katika viwanja hivyo.
Walipoulizwa sababu ya kumzomea mbunge huyo,
baadhi wa wananchi walisema hawana imani naye wakidai alichakachua
matokeo ya mwaka 2010.
Mmoja wa wananchi hao, Mohamed Said alisema
alipofika katika ofisi za halmashauri, dhana iliyomjia kichwani ni
uchakachuaji. Aliongeza kuwa kuwapo kwa Dk Mahanga kungesababisha vurugu
kubwa bila sababu.
“Mbona katika maeneo mengine wanakoapishwa wenyeviti wabunge wao hawajaenda, yeye amefuata nini?” alihoji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Hali ya ulinzi
Utata wa matokeo
Kama ilivyokuwa juzi katika Manispaa ya Kinondoni
ambako ilidaiwa kuwa baadhi ya wagombea walioshinda hawakuitwa kuapishwa
lakini wakaitwa wasioshinda, vivyo hivyo katika Manispaa ya Ilala mambo
yalikuwa hayohayo, tofauti ni kuwa hayakurushwa mabomu ya machozi wala
risasi.
Jana, madudu zaidi yalibainika katika baadhi ya
kata na mitaa, tofauti na juzi, uapishaji uliahirishwa hadi mgogoro
uliojitokeza upate suluhisho.
Baadhi ya majina yaliyoibua utata ni Mariano
Maurus, mgombea uenyekiti wa CCM, Mtaa wa Kigogo Fresh B na Ubaya Chuma,
aliyekuwa mgombea wa CCM, Mtaa wa Migombani, Kiwalani.
Aliyekuwa mgombea uenyekiti Mtaa wa Kigogo Fresh B
kupitia CUF, Patricia Mwamakula alisema uchaguzi katika mtaa huo
ulivurugika na mshindi hakupatikana licha ya kuwa alikuwa amemwacha
mbali mpinzani wake.
Alisema siku hiyo fujo zilitokea, masanduku ya
kura yakachomwa moto kabla ya matokeo kutangazwa na baadaye
walibandikiwa matangazo kuwa uchaguzi ungerudiwa Jumapili iliyofuata
lakini mpaka jana haukuwa umefanyika.
“Tunashangaa kuona mgombea wa CCM anaitwa kula
kiapo wakati nilimshinda na hawakutoa matokeo baada ya uchaguzi
kuvurugika. Lazima haki itendeke, hatutakubali ufisadi huu,” alisema
mama huyo.
Hata hivyo, Maurus ambaye aliitwa jina kula kiapo,
alisema ndiye mshindi halali wa Mtaa wa Kigogo Fresh B. Alisisitiza
kuwa uchaguzi ulifanyika vizuri na kura zikahesabiwa kabla ya vijana
kuanzisha fujo na kuchoma masanduku ya kura.
“Wakati vurugu zinatokea, wasimamizi walikuwa
tayari wamehesabu kura. Masanduku yaliyochomwa moto yalikuwa
yamehesabiwa. Tumezoea kelele za hawa wapinzani, hawana jipya,” alisema
Maurus.
Lilipoitwa jina la Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani
– Kiwalani, Chuma watu walianza kupiga kelele kupinga jina hilo.
Mwenyekiti huyo alipojitokeza kuingia ukumbini, wananchi walimvuta na
kuanza kumpiga.
Hata hivyo, Chuma aliokolewa na askari waliokuwapo
na kupelekwa katika chumba kimoja ili kumnusuru. Alikaa humo muda wote
wakati wengine wakiendelea kuapishwa.
Mjumbe wa mtaa huo, Ramadhan Miroba alisema
mgombea uenyekiti wa CUF, Kassimu Mshamu alikuwa na nafasi ya ushindi
ndiyo maana wananchi wamepinga jina la huyo mgombea wa CCM.
“Uchaguzi ulivurugika dakika za mwisho kabla matokeo
hayajatangazwa, kilichosababisha vurugu siku ya uchaguzi ni masanduku ya
kura ya kata ya Vingunguti kukutwa mtaani kwetu,” alisema mjumbe huyo
kupitia CUF.
Utata Pugu Kwalala
Katika Mtaa wa Pugu Kwalala, mwenyekiti mteule,
Dorkas Lukiko alishuhudia majina ya watu wasiostahili yakiitwa kuapishwa
kama wajumbe wake badala ya wale walioshinda uchaguzi.
“Licha ya mimi kushinda nafasi hii wapo wajumbe
watatu wa Chadema na wawili wa CCM lakini nashangaa majina yote
yaliyoitwa katika nafasi ya ujumbe ni ya watu wa CCM pekee, tena mmoja
wao ni yule niliyechuana naye katika uenyekiti,” alisema Lukiko na
kuongeza kuwa wote wasiostahili hawakuwapo kwa kuwa wanajua kuwa
hawapaswi kuapishwa.
Hata hivyo, baadaye majina hayo yaliyosomwa yalifutwa na wale wajumbe watatu wa Chadema kuapishwa.
Kata tano zawekwa kiporo
Kutokana na utata uliojitokeza katika mitaa hiyo
miwili na maeneo mengine, Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Mashauri
Musimu alitangaza kusimamisha viapo kwa wenyeviti na wajumbe wa kata
tano za Jimbo la Segerea kati ya 35. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Nimeshauriana na mkurugenzi naye ameniambia
niwaambie mchague moja kati ya kuendelea na uapishaji wajumbe mliopo au
kusitisha mpaka pale uongozi utakapojiridhisha na wanaostahili.
Kutoapishwa leo hakumaanishi kuwa hamtambuliki kisheria kwani ninyi ni
viongozi halali katika maeneo mtokayo,” alisema Musimu.
Kabla ya kutangaza kuahirisha, Musimu aliwaeleza
wafuasi wa vyama waliokuwapo kuwa shughuli hiyo itakamilishwa bila
kuhusisha mitaa mitatu yenye utata, jambo lilizua tafrani kwa wafuasi wa
Ukawa ambao waliwataka viongozi wao wasishiriki.
“Taarifa zilizopo ni kwamba katika Mtaa wa Segerea
-Migombani uchaguzi haukufanyika na watapangiwa tarehe ya kurudia
wakati Kigogo Fresh B wamekuja watu wawili. Kiwalani - Migombani ni haya
mnayoyakataa, yote haya yanahitaji kujiridhisha kabla hatujayatolea
uamuzi ingawa tunaweza tukaendelea na wale waliopo,” alisema Musimu.
Baada ya kauli hiyo wafuasi wa Ukawa walisimama na
kutaka kutoka nje ya ukumbi lakini polisi waliwashawishi wabaki ndani
kupata suluhu ili kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea.
Hali ya ulinzi
Kutokana na umati uliokuwapo, polisi walisoma mchezo na kuandaa
utaratibu wa kuita majina ya wajumbe wote waliotakiwa kuingia katika
ukumbi huo, tofauti na hali ilivyokuwa juzi Kinondoni.
Kilichokuwa kinafanyika ni kuita jina la mwenyekiti wa mtaa husika ambaye alitakiwa kuwatambua wajumbe wake ili waingie ndani.
Kutokana na udogo wa ukumbi, wajumbe hao
walilazimika kuingia kwa awamu kulingana na majimbo yao na ilipofika
zamu ya Segerea kwa wingi wa mitaa yake nao walilazimika kuingia kata
moja baada ya nyingine.
Shughuli hiyo ilifanyika kwa mafanikio katika
awamu mbili za kwanza lakini ilipata kikwazo katika awamu ya tatu baada
ya kelele nyingi za wafuasi wa Ukawa kushinikiza isitishwe mpaka pale
dosari zitakaporekebishwa.
Kata tano ziliathirika na usitishaji huo ambazo ni
Kimanga, Kisukuru, Liwiti, Kinyerezi pamoja na Segerea kutokana na
utata uliojitokeza katika mitaa mitatu ya Kiwalani - Migombani, Segerea -
Migombani na Kigogo Fresh B ambako kulikuwa na utata wa matokeo.
Baada ya kusitishwa, wafuasi wa Ukawa waliokuwa
wamewasindikiza wagombea wao walishangilia na kuimba nyimbo za
kujipongeza kwa kufanikisha kile walichokiita kuzuia unyongaji wa
demokrasia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment