Thursday, January 08, 2015

FERNANDO TORRES AREJEA KWA KISHINDO

Fernando Torres  
 
Fernando Torres arejesha ushindi katika klabu yake ya Atletico Madrid kwa kuwabamiza Real Madrid 2-0 katika michuano ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Mbele ya umati wa mashabiki 46,800 waliokuwa wakiishuhudia mechi hiyo ya aliyekuwa mchezaji mahiri wa timu za Liverpool na Chelsea, amerejea katika timu yake iliyomkuza na kumtambulisha kipaji chake, Atletico Madrid.
Raul Garcia,aliipatia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 58 akifunga kwa njia ya penalti, huku Jose Maria Gimenez akikamilisha ushindi wa Atletico kwa kufunga bao kwa njia ya kichwa katika dakika ya 76 ya mchezo.
Torres mwenye miaka 30 alibadilishwa katika dakika ya 59. Mchezaji aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka katika timu ya Italia ya AC Milan wiki iliyopita, ndiye aliyeongoza kwa ufungaji katika timu ya Atletico kwa misimu mitano kabla hajatia mguu Liverpool mwaka 2007.
Mashabiki wapatao 45,000 waliishuhudia mechi iliyopigwa katika uwanja wa Vicente Calderon mnamo siku ya Jumapili wakati ambapo utambulisho wa Torres ulipofanyika na papo hapo jezi zenye jina lake zikaanza kuuzwa ambapo ndani ya saa 24, ziliuzwa jezi 2,000. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...