Wednesday, December 31, 2014

BOSI UEFA AISHAURI FIFA KURUHUSU KADI NYEUPE UWANJANI

Soccer - Michel Platini File Photo

Rais wa UEFA Michel Platini amesisitiza mpango wake wa kuanza matumizi ya ‘Kadi Nyeupe’ itakayowafanya wachezaji watolewe nje kwa muda kisha kurejeshwa baadaye. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 59 alitoa wazo hilo kwa mara ya kwanza Oktoba lakini likapingwa na Rais wa FIFA Sepp Blatter.
Hata hivyo, Platini ameshikilia msimamo wake katika mkutano wa tisa wa kimataifa wa michezo unaofanyika Dubai.
“Kadi nyeupe ni kitu kipya. Inahusiana na tabia ya wachezaji wa soka. Kujiangusha na kujifanya kuumia, kupinga maamuzi ndani ya uwanja, haya hayakubaliki kwa watu wanaopenda mchezo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Kadi ya njano itaendelea kutumika pia lakini inavutia zaidi kuwa na kadi nyingine.
“Hii kadi nyeupe itamtoa mchezaji ndani ya uwanja kwa dakika kadhaa, kama tano au 10. Hii itasaidia kuufanya mchezo upendwe na watu wasiopenda kitendo husika.
“Tukiwa na kadi nyeupe, hakutakuwa na kufukuzwa uwanjani. Ninafikiri tunapaswa kujifunza kwenye michezo mingine, kama ‘rugby’, ambao wanatumia mfumo huu.”
Mchezaji huyo wa zamani wa Nancy, Saint-Etienne na Juventus, ambaye aliiongoza Ufaransa kutwaa ubingwa wa Ulaya 1984 na kutinga mara mbili nusu fainali za Kombe la Dunia, amesemaSheria ya Kuotea (Sheria Namba 11 ya Soka) inapaswa kurahisishwa ili ieleweke kwa watu wengi zaidi.
“Kuna aina na taratibu nyingi za kuotea. Ni vigumu kupata aina moja na isiyokiuka miiko kutafsiri sheria ya kuotea. Inabidi tuwaruhusu watu walioko mbele ya kamera kujua kuotea pia,” ameongeza Platini.
“Sasa tunahitaji kuishawishi FIFA”.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...